Bembea: Maudhui ya Mabadiliko

mabadiliko

¾    Mabadiliko yanajitokeza pale ambapo Yona anatueleza kuhusu maisha yake ya ujana alipokuwa mwalimu. Anatueleza namna alivyokuwa akiamka alfajiri na mapema kiboko mkononi na mwanafunzi aliyekuja baada yake angepokea kichapo. Anasema kuwa siku hizi huwezi kumnyoosha mtoto kwa kiboko. Suala hili linamaanisha kuwa kuna mabadiliko ya sheria na kanuni za shuleni (uk. 62).

¾    Suala la mabadiliko linadhihirika wakati Yona anakubaliana na Sara. Mtazamo wa Yona kwa Sara unabadilika. Alikuwa hana huruma kwa mkewe Sara alipokuwa mgonjwa. Katika onyesho la kwanza, Yona analalamika kwa sababu Sara alikuwa hajamwandalia chakula. Yona alikuwa hana huruma hata baada ya Sara kumwelezea kuwa alikuwa hajaandaa chakula kwa sababu ya maumivu (uk. 1).

¾    Mabadiliko yanajitokeza wakati Yona anaonekana kuhuzunishwa na maradhi ya mke wake. Anasema aliona hapo awali kama maradhi yale yalikuwa mchezo lakini sasa anatamani angeishi tofauti. Yona anasema hawezi kuendelea kuishi kama zamani, ni lazima angefuata mkondo mpya wa maisha. Anataka kuzitumia siku zake za uzee kumshughulikia mkewe (uk. 70). Anamwambia Sara pole na kusema kuwa taabu zake Sara zitakuwa taabu zake (uk. 74).

¾    Yona amesawiriwa kukuza maudhui ya mabadiliko. Mwanzoni, ameonyeshwa kama mtu mzuri, baada ya kusutwa na kudharauliwa kwa kukosa mtoto wa kiume anabadilika na kuwa mlevi na kupoteza upendo kwa familia yake. Tunamwona akimpokeza bibiye kichapo cha mbwa hadi kusababishia bibiye maradhi ya moyo. Yona anabadilika kutoka hali hiyo ya ulevi kwa kuamua kuchukuwa mkondo mpya wa maisha (uk. 70). Anasema kwamba pombe imemchezesha kama mwanasesere na kumnyima fursa ya kuilea familia yake.

¾    Kuna mabadiliko ya mitazamo ya utamaduni wa jamii ya kizazi cha jana na ya kizazi cha leo. Mabadiliko haya yanajidhihirisha kupitia suala la mtoto wa kike na mtoto wa kiume. Mtazamo wa mtoto wa kike katika kizazi cha jana umebadilishwa na utamaduni wa kizazi cha leo. Kizazi cha jana kinamwona mtoto wa kike kama mtoto asiyekamilika na asiyestahili kusomeshwa wala kurithi mali ya familia (uk. 60). Wazo hili linabadilishwa na kizazi cha leo ambacho kinamwona mtoto wa kike sawa na mtoto wa kiume. Kwa hivyo, kama mtoto wa kiume, yeye pia anaweza kurithi mali ya familia na vilevile kusomeshwa.

¾    Kuna mabadiliko ya mitazamo ya utamaduni wa jamii ya kizazi cha jana na ya kizazi cha leo. Mabadiliko haya yanajidhihirisha kupitia suala la mtoto wa kike na mtoto wa kiume. Mtazamo wa mtoto wa kike katika kizazi cha jana umebadilishwa na utamaduni wa kizazi cha leo. Kizazi cha jana kinamwona mtoto wa kike kama mtoto asiyekamilika na asiyestahili kusomeshwa wala kurithi mali ya familia (uk. 60). Wazo hili linabadilishwa na kizazi cha leo ambacho kinamwona mtoto wa kike sawa na mtoto wa kiume. Kwa hivyo, kama mtoto wa kiume, yeye pia anaweza kurithi mali ya familia na vilevile kusomeshwa.

¾    Mabadiliko ya utamaduni pia yanajitokeza katika suala la ndoa. Sara anamweleza Asna kuwa zamani, wasichana walikuwa wakiozwa punde tu walipobaleghe (uk.52). Mtindo huu unabadilika miongoni mwa kizazi cha leo kwani wasichana wanaolewa wakati watakapo.

¾    Mabadiliko ya utamaduni yanadhihirika kutoka kwa mhusika Yona ambaye, hapo awali, hangeweza kuingia jikoni kumpikia mkewe Sara. Baada ya kugundua kuwa hayo ni mambo yaliyopitwa na wakati, tunamwona akiandaa kiamshakinywa kwa familia yake. Pia, anamhakikishia Sara kuwa atamshughulikia kwani hali yake Sio nzuri (uk. 62).

¾    Kuna mabadiliko ya mitazamo au uonevu wa mambo katika tamthilia hii. Neema anabadilisha mtazamo wake kuhusu baba yake (uk. 72).

¾    Bunju pia anabadilisha mtazamo wake wa kutomsaidia Neema kugharamia matibabu ya mamake Sara. Anamwambia anaenda kukutana na mkurugenzi wa kampuni na kuwa akipata hela, atampiga jeki katika suala la matibabu ya mama yake (uk. 40).

¾Tamthilia ya Bembeaya Maisha inaangazia mabadiliko ya maisha. Mabadiliko haya yanajitokeza kupitia familia ya Yona. Kwanza, maisha ya Sara, mkewe Yona, yanabadilika kutoka kuwa ya afya njema na kuwa yenye afya duni. Afya ya Sara inazorota kutokana na ugonjwa wa moyo ambao ataishi akimeza vidonge vya dawa maisha yake yote (uk. 71).

¾    Pia, mtazamo wa wanajamii kuhusu familia ya Yona unabadilika pia. Wanajamii sasa wanaiheshimu familia ya Yona ambayo ilikuwa imedharauliwa na kudunishwa hapo mbeleni. Familia hii haisutwi wala kutukanwa kwa sababu ya mafanikio na elimu ya mabinti wao. Jambo hili linadhihirishwa kupitia maneno ya Luka wakati walikuwa wakiongea na Beni na Yona.