1. Dondoa sauti mwambatano zilizo kwenye maneno haya kisha utaje mahali pa kuzitamkia;
i) ngao /ng/- kaakaa laini
ii) avya /vy/- meno
2. Tambua muundo silabi katika neno MAKTABA
KIKKIKI
3. Eleza sifa mbili mbili za sauti zifuatazo
/i/
-Irabu ya mbele ya ulimi/hutamkiwa mbele ya ulimi.
- Inapotamkwa midomo hutandaza.
/o/
- Irabu ya nyuma ya ulimi / hutamkiwa nyuma ya ulimi.
- Inapotamkwa midomo huviringa.
4. Onyesha mahali mkazo unapowekwa kwenye neno ‘Tenganisha’
– Tenga‘nisha/ tenganisha
5. Eleza matumizi manne ya kiimbo.
– Kutolea rai/wazo
- Kuuliza swali.
- Kuonyesha amri/kuamrisha.
- Kuonyesha mshangao.
6. Andika tofauti mojamoja kati ya sauti.
/ny/ na /y/
/ny/ ni king’ong’o ilhali /y/ ni kiyeyusho/nusu irabu
/g/ na /gh/
/g/ ni kipasuo ilhali /gh/ ni kikwamizo.
7. Andika tofauti moja kati ya sauti zifuatazo
i. /ny/ na /y/
/ny/ ni king’ong’o ilhali /y/ kiyeyusho
ii. /d/ na /t/
/d/ ni ghuna ilhali /t/ sighuna
iii. /mb/ na /nd/
/mb/ ni sauti ya midomo ilhali /nd/ ni ya ufizi
iv. /s/ na /z/
/s/ ni sighuna ilhali /z/ ni ghuna
8. Taja sifa moja linganishi kwa sauti /t/ na /l/.
-Ni sauti za ufizi.
9. Huku ukitoa mifano, eleza miundo miwili ya silabi mwambatano
i)KKI-nyumba
ii)KKKI-mbweha
Andika neno lenye sifa zifuatazo; Kipasuo ghuna cha ufizi, irabu ya kati, kipasuo sighuna cha ufizi, irabu itamkwayo midomo ikiwa imetandazwa
-data
10. Taja sauti zifuatazo:
i) Kikwamizo sighuna cha ufizi (alama 1)
/s/
ii) Nusu irabu ya kaakaa gumu (alama 1)
/y/
11. Ni sauti gani haifai kuwa miongoni mwa hizi. Toa sababu (alama 2)
i. /ng’/ /g/ /t/ /k/
Sauti /ng’/ ni king’ong’o ilhali zingine ni vipasuo
ii. /s/ /v/ /ch/ /sh/
Sauti /ch/ ni kizuio kwamizwa ilhali izingine ni vikwamizo
12. Taja sauti zilizo na sifa zifuatazo: (Alama 2)
(i) sauti ya wastani na nyuma ya ulimi
/o/
(ii) kikwamizo cha ufizi
/z/
(iii) hutamkiwa koromeo
/h/
(iv) hutamkwa ncha ya ulimi inapojipigapiga haraka kwenye ufizi
/r/
13. Andika neno lenye sauti zifuatazo (alama 1)
Kipasuo-kwamizo sighuna cha kaakaa gumu,irabu ya juu,nyuma,irabu ya juu,nyuma ,kikwaruzo ghuna cha masine,irabu ya chini,kati tandaze
-chuuza
14. Dondoa sauti mwambatano katika maneno yafuatayo na uainishe mahali pa kutamkia. (alama 1)
Tamba
/mb/ midomo
Afya
/fy/ midomo-meno
15. Linganua irabu katika neno; mavue. (alama 1)
/a/ chini, kati tandazi
/u/ sauti ya nyuma juu virigwa
/e/ sauti ya mbele wastani, tandazi