Mawali na Majibu-Mapambazuko ya Machweo

1. Mume wangu, ninapoandika waraka huu, naomba uelewe kuwa wanao wawili wanazidi kuumia. Labda unadhani unayoyafanya ni siri ila usilolijua ni kwamba kila ufanyalo nalifahamu.

a) Fafanua muktadha wa dondoo hili (alama 4)

 Ni maneno ya Bi suluhu katika barua kwa mumewe,

 Yaliyosomwa na Abigael

 Alikuwa kwenye chumba walipopatana Abigael na Bw. Suluhu.

 Barua ilikuwa ya kumjulisha Suluhu kuwa yote aliyoyafanya yalijulikana

b) Tambua umuhimu wa mandhari katika dondoo hili katika kujenga maudhui (alama 4)

 Yachimuza maudhui ya uzinifu- Suluhu anashiriki mapenzi nje ya ndoa na wasichana wadogo.

 Maudhui ya uozo- Bw. Suluhu ana wapenzi wengi na ambao ni wachanga. Anashiriki mapenzi na Abigael bila kujali kuwa atamwambukiza ugonjwa.

 Kuimbua maudhui ya Unafiki- Suluhu anafikiri anapendwa na Abigael na hata kufikiri kumwoa ilhali Abigael anajifanya na hata kupanga kumuua.

 Ukatili- Abigael anaisagasaga dawa kwa nia ya kumpa Suluhu ili apate nafasi ya kumuua./ kuteguliwa kwa kitendawili cha kifo cha mamake

 Mapenzi- Suluhu anampenda Abigael na alitamani hata waoane. Anajiona kama mfalme wakiwa na Abigael.

 Majuto- Abigael anajutia kuingilia ndoa ya Suluhu na mkewe baada ya kusoma kisa cha Bi. Suluhu.

 Uwajibikaji- Abigael anaamua kuwajibikia maisha yake baada ya kusoma barua.

 Barua ile ilifichua kutowajibika kwa Suluhu kwa familia, wananchi waliomchagua na kwa Abigael kwa kutomwambia ukweli kuhusu afya yake.

c) Bainisha hulka nne za mzungumzaji (alama 4)

Sifa za Bi. Suluhu

 Mvumilivu- anavumilia kusalitiwa kimapenzi na Suluhu Msiri- hakumwambia yeyote siri z amumewe alizojua Mwajibikaji- aliweza kujitahidi na kuwalea wanawe peke yake.

 Mwadilifu- ansema angeweza kumfanyia mumewe mengi hata kumpa sumu ila hakuyafanya

 Mpelelezi/mpekuzi- anafanya uchunguzi wake na kujua mahusiano ya mumewe

 Mshauri mwema- anamshauri Suluhu kumwambia Abigael ukweli

 Mwenye mapenzi- alimpenda mumewe

d) Onyesha toni inayojitokeza katika dondoo hili (alama 2)

 Toni ya uchungu- anaumwa kuwa watoto wake wanaumia kwa matendo ya mumewe.

e) Dhihirisha kuwa kila alilolifanya mumewe lilijulikana (alama 6)

Alijua kwamba:

 Yule binti wa chuo kikuu aliyepanga ahitimu kabla ya muda wake aliishia kumtunga mimba na kumwacha bila tumaini.

 Hata yule hawara mwingine aliyeishia kumpangia chumba kule mjini ili asijue alimwambia kila kitu.

 Alimuua mama Abigael ila hakuwaambia polisi

 Alinyakua shamba la mamake Abigael.

 Alifuja pesa za wananchi kwa kuwalipa wasichana wa vyuo vikuu baada ya kula uroda nao.

 Alishindwa kuleta maendeleo kwa kuwa alitafuta mbinu ya kumlipa Bw. Ngoma pesa alizomkopesha za kampeni ya ubunge.

 Kuwa hajamwambia Abigael kuwa ameugua

2. “Poko! Ukiumwa na nyuki haina haja ya kujitwika jukumu la kuharibu mizinga yote ya asali. Hujui faida ya nyuki ulimwenguni? Uliamua kuharibu asali ya nchi.

Jadili maudhui ya ukiukaji wa haki za watoto katika hadithi ya ; i.

i. Mapambazuko ya Machweo (alama 10)

 Haki ya kuishi/ jasho- hakuna hewa mgodini

 Ajira ya watoto- watoto wadogo na vijana kuchimba mchanga na kusomba kwa mikokoteni.

 Afya – hakuna miale ya jua kwenye mgodi  Kutishwa na wanyapara- walinzi katili

 Mazingira duni

 Kuchimba gizani- taa za vibatari

 Kulala kwenye mabanda

 Kutoruhusiwa kuondoka- walinzi wakali, mbwa wakubwa na nyua za stima

 Kukatiziwa masomo- vijana na watoto wadogo

 Wanakusanywa barabarani kwa probox ya Makutwa

 Kufanywa kuwa watumwa- Sai na Dai

ii. Sabina (alama 10)

 Kunyimwa haki ya kusoma- anaambiwa anaharibu mafuta na Yunuke

 Kukatiziwa masomo- Nyaboke kuacha shule katika kidato cha pili

 Ndoa za mapema – Nyaboke kukataa posa za wanaume/ Sabina kuozwa siku ya kutangaza matokeo

 Kufanywa mtumwa- kazi zinazozidi umri wa Sabina/ miaka 14

 Mavazi kuu kuu- Sabina kutoka shambani akiwa na rinda kuu kuu  Mateso- matusi ya Yunuke, kumzimia taa, kumkashifu kwa kutouuza maziwa Itumbe

 Kuchelewa kufika shule- anafika saa tatu na nusu

 Kudhalilishwa – kukama ng’ombe, kuwapeleka malishoni, kuzoa kisonzo, kuuza maziwa asubuhi,kuandaa chajio, kuwafunga ng’ombe zizini

 Kutolindwa dhidi ya hatari – watu kuambaa familia ya Nyaboke/ laana

 Kudharauliwa na binamu zake Sabina/ Mike ndiye anambebea vitabu wakiwa malishoni.

 Kujaribu kumnyima bahati kwa kumwita Mike kuhojiwa na wanahabari.

3. Siku moja alipokataa katakata kuandamana na mumewe, jungu lilifoka. “Wewe mke sampuli gani usiyetaka kumuunga mkono mmeo?” Haya kaa nyumbani. Kula na kulala tu, hujui jingine. Ona umbo lako sasa, kama nguruwe. Si mke mrembo niliyeoa! Wanawake ni wengi…”

a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)

 Msemaji ni Luka

 Msemewa ni Lilia  Nyumbani kwao

 Luka alimtaka mkewe kuandamana naye katika kampeni

b) Bainisha vipengele vinne vya kimtindo katika dondoo hili (alama 4)

 Balagha – wewe mke sapuli gani?

 Nahau = katakata, unga mkono

 Taswira – ona sasa  Tashbiha – kama nguruwe

 Masimango – kama nguruwe

 Nidaa – niliyeoa!

 Mdokezo – wengi…

c) Fafanua nafasi ya mwanamke katika hadithi hii. (alama 12)

 Mwanamke kutawishwa- lilia anaachishwa kazi ya umeneja na mwishowe kutawishwa.

 kukaa nyumbani na kutishwa asidhubutu kutoka nje ya lango.

 Mwanamke anatishiwa – Lilia anapodhubutu kumshtaki mumewe anakumbushwa kuwa yeye ndiye Gavana na ana uwezo wa kufanya haki kuwa batili na batili kuwa haki.Utajua kichomtoa kanga manyoya.

 Mwanamke anapokezwa kichapo cha mbwa- Lilia anapokea mapigo kutoka kwa mumewe anapoenda kuripoti kwa polisi.

 Mwanamke kutusiwa- Lilia anaambiwa amenona kama nguruwe.

 Mwanamke kudhalilishwa- Lilia annambiwa kuwa ana umbo kama nguruwe kwani kazi yake ni kula na kulala tu.

 Mwanamke kuendewa kinyume na mumewe katika ndoa- Luka anasemekana kuwa na kiruka njia ambaye waliandamana naye kila mahali. Lilia anapouliza ni nani anapokea kipigo kinachomlaza kitandani siku mbili.

 Kuachishwa kazi. Lilia anaachishwa kazi na mumewe ili awe mpokezi wa wageni nyumbani.

 Ni chombo cha starehe-

 Wasaliti – kunyanganywa bwana

 Kunyimwa uhuru wa kutangamana

 Kutohusishwa katika maamuzi ya familia

 Mwajibikaji – mamake gavana

 Mwaminifu – Lilia kwa mumewe

 Mwenye mapenzi ya dhati- Lilia

 Mvumilivu- Lilia na mavya wake

4. (a) Changanua mtindo katika kifungu hiki kutoka hadithi ya Fadhila za Punda (alama 10)

Aligutuka kutoka kwenye usingizi wa mang‟amumang‟amu, roho mkononi, pumzi zikimwenda mbio. Hakujua kilichomwamsha,hivyo alitega sikio ndi!...Labda ghamidha itakuwa imezidi, imefura kama hamri lililotiwa hamira… Saa ya ukutani ilimwambia saa nane za usiku, wakati waja wamelala, misono tu,…alipoiona hiyo missed call akajua basi…Aliamka kuelekea kitandani kuuhitimisha usiku wake kwa sababu ni wazi mgeni haji tena. Akawa anapita kioo kwenye verenda . Chenyewe kimepasuka…mbona ikawa hivi?Mbona Luka kageuka kuwa kuwa mzigo wa moto, habebeki, habebeki kamwe?

 Taharuki- Aligutuka kwenye usingizi wa mang’amumang’amu

 Tashhisi –pumzi zikimwenda mbio

 Tanakali za sauti- hivyo alitega sikio ndi!

 Tashbihi- imefura kama hamri lililotiwa hamira

 Taswira- Saa ukutani ilimwambia saa nane usiku, misono tu

 Kuchanganya ndimi- alipoiona hiyo missed call

 Kejeli- mgeni haji tena

 Swali balagha- Mbona ikawa hivi?

 Takriri Habebeki, habebeki kamwe?

 Jazanda- mzigo wa moto

(b) Fafanua dhiki zinazowakumba raia katika hadithi ya Msiba wa Kujitakia (alama 10)

 Ukosefu wa ajira. Raia kama vile Machoka wamechoka kutafuta kibarua mchana kutwa bila mafanikio

 Njaa. Machoka hajayia chochote kinywani tangun asubuhi kiasi kwamba matumbo yake kushindwa kuhimili makali ya njaa

 Ukabila. Zuhura anamsisitizia Machoka kuwa wampigie kura sugu junior kwa sababu ni wa kabila lao

 Tofauti za kisiasa. Zuhura na Machoka hawapatani kwa sababu wote wawili ni wafuasi wa wawili tofauti kisiasa

 Hali ngumu ya kiuchumi. Wanamatopeni wanapitia hali ngumu ya maisha kwa mfano mfumko wa bei za bidhaa na kutozwa ushuru wa kiwango cha juu na serikali

 Kupuuzwa na viongozi baada ya uchaguzi

 Hongo na vishawishi vingine. Kina Zuhura wanashawishiwa kwa kanga, sukari na unga wa sima

 Biashara duni- Wanamatopeni wanalipwa mishahara duni amabayo haiwezi kukidhi mahitaji yao

 Kufungwa gerezani. Mzee Sugu Senior alifungwa gerezani na walowezi kwa kupigania ukombozi wao

 Vingozi wa kinasaba. Ni aila mbili tu ndizo zimekuwa zokizozania uongozi wa Matopeni tangu uhuru wa jimbo hilo.

 Wanasiasa wa upinzani wanaendeleza kampeni kwa kupuuza sera na maendeleo yanayodaiwa na serikali

 Kura zinazopigwa kwa misingi wa kinasaba/ kikabila. Zuhura anampigia Sugu Junior kura kwa vile ni wa kabila lake.

 Wafuasi wa wanasiasa tofauti hawapatani. Machoka na Zuhura hawakuwa wakielewana kwenye kipindi cha siasa kwa vile Machoka alimuunga Fumo Matata huku Zuhura akimuunga Sugu Junior.

 Wapiga kura wanarauka asubuhi ya majogoo, wakastahimili baridi na jua kali ya mchana

 Wanamatopeni wanalimbikizwa viongozi wasiotaka kuhusisha watu kupiga kura , kuhesabu kura kwa kuwapendelea vigogo serikalini.

 Uhuru wa vyombo vya habari kubanwa. Vyombo vyote kupeperusha mubashara hafla ya kuapishwa kwa Sugu Junior

 Ubadhirifu wa mali ya umma. Mali ya serikali ya Matopeni zinatumiwa kugharamia safari za ndge za viongozi wote wa majimbo jirani.

 Kulimbikizwa viongozi, udikteta na ukoloni mamboleo. Kahindi anadai kuwa vizingiti hivi haviishi daima Matopeni

5. “ Alishangaa kwa nini wakati wote huu hakuna mtu aliyejua shughuli ile dhalimu iliyokuwa ikiendelea.”

a) Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4)

 Mnenaji ni mzee Makucha

 Anajiambia/ anaiambia nafsi yake

 Alikuwa kwenye migodi iliomilikiwa na mzee makutwa(Mamboleo)

 Anashangaa ni vipi hakuna mtu aliyejua shughuli ile dhalimu iliyokuwa ikiendelezwa na mzee Makutwa

b) Huku ukitoa mifano mwafaka, eleza jinsi ambavyo haki za watoto zimekiukwa katika hadithi ya Mapambazuko ya Machweo (alama 8)

 Mzee Makutwa anawarundika watoto wa kiume kuwapeleka kusikojulikana na baada ya kupelekwa huko hawaruhusiwi kutoka

 Mzee Makutwa anawatumia vibaya vijana wa mitaani, walevi na wavuta bangi, watoto wa kikopo

 Riziki, binti wa kipekee wa Mzee Makucha anaolewa akiwa na umri mdogo na kigogo mhindi ughaibuni japo babake anashikilia alitoroshwa si kuolewa

 Baadhi ya vijana wadogo(watoto) wameajiriwa kuwa madereva wa probox ya mzee Makutwa

 Watoto wadogo mno wenye umri wa miaka chini ya kumi wameajiriwa kudondoa vijiwe vidogovidogo vyenye kungaa mgodini

 Vijana na watoto wadogo mno wanafanyizwa kazi na wanyapara wanaoamrisha kwa sauti ya kutisha

 Vijana mabarobaro wanafanyizwa kazi ya kuusukuma matoroli yaliyoshiba mchanga kutoka pangoni

 Vijana wadogo walijisulubisha pangoni kuchimba madongo kwenye mazingira ya joto jingi na uhaba wa hewa  Watoto na vijana waliokuwa wakihangaishwa na urumo/ ukata walichukuliwa na Mzee Makutwa akiwakatishia masomo

 Vijana hao wadogo walivalia mavulia ambayo Mzee Makutwa aliwazolea majiani  Riziki waliyopata watoto hao ni mshahara mdogo

 Vijana hao walilala kwenye mabanda yaliyojengwa kigugu

 vijana walifungiwa mgodini wasitoke kwa kuzungushiwa ua wa stima

 Hata baada ya kushikwa, Mzee Makutwa anaapa kuwarejesha mgodini vijana waliokwisha kutorokea msituni.

c) Jadili athari za suala linalorejerelewa katika dondoo hili kutoka hadithi ya Kila Mchezea Wembe (alama 8)

“Sikupita kwingine. Nilishika tariki moja kwa moja hadi…Huko nilikuta tayari yamechacha…”

 Kupofuka- Tembo anasema baadhi ya walevi walipofuka

 Kukosa hamu ya chakula- Tembo anasema hana hamu ya chakula tangu siku hiyo

 Kupoteza hisia za mguso-Tembo alipoteza hisia .Zilirudi baada ya matibabu

 Kupoteza damu- Tembo alibubujikwa na damu puani baada ya kunywa pombe yenye sumu

 Kutapika –Tembo alianza kutapika baada ya kunywa pombe yenye sumu  Upweke-Tembo anasema maisha yake hospitalini yamekuwa magumu

 Kushushwa cheo kazini

 Kukosana na wazazi

 Kakataliwa

 Fujo nyumbani- alileta fujo katika matanga

 Kukosa heshima. Aliwakosea wafu

 Majuto- anajutia matendo yake

 Matusi- Emmi anasema Tembo alitusiana akiwa mlevi

 Mapuuza –Emmi analalamika kuwa Tembo alitelekeza familia yake

 Kuvunjika kwa familia- Emmi anavunja ndoa yake na Tembo

 Kutozingatia usafi-mazingira ya mamapima

 Vifo- Moshi anakufa kwa sababu ya kunywa pombe haramu

 Kufungwa- Mamapima anafungwa baada ya kifo cha Moshi

6. Tukaangaliana. Hapo nikaanza kuukagua mwili wake Naisoma hasa. Akanishika mkono kunisaidia kusimama. Nikaitikia. Moyo ukamridhia huyu mridhia wa muda. Mwendo wa aste aste mpaka alipokuwa ameegesha gari. Tukapiga selfie. Takawa kama tumejuana kwa muda mrefu. Nyoyo zetu zikakurubiana. Akanifungulia mlango wa gari. Tukatifua vumbi la beach na kuondoka. Sijakutana na mwanamume kama huyu, pengine kuona kwenye sinema! Alikuwa wa asili ya kiarabu. Mweupe, macho yake ya wastani meupe kama theluji ila malegevu. Uso wenye umbo la embe dodo, kidevu kimenyolewa vizuri utadhani kimechongwa na kuacha uso kung'aa Nwyele za singa zinanukia udi hasa. Mwili wote unanukia riha ibura ya uturi Mikono imechongeka vizuri kwa misuli ya wastani Kifua nacho ni cha ngao! Usiseme maguu manene yaliyoketi vizuri kwenye kaptura lake la buluu Alikuwa hana tenge huyu Nikajipata nimenasika hapo usoni, naye akaniangalia akitabasamu. Ndipo nikaona meno yaliyojipanga vizuri, meupe ya kuacha mwanya wa kutia nakshi tabasamu lake. Ngozi yake imetepweka kama jejeta.

a) i)Eleza aina za taswira katika utungo huu (alama 5)

 Taswira oni- tukaangaliana

 Taswira mguso-Akanishika mkono...

 Taswira sikivu- Nikaitikia

 Taswira mwendo-Mwendo wa astcaste..

 Taswira hisi -Nyoyo zetu zikakurubiana

 Taswira mnuso- Mwili wote unanukia riha ibura ya uturi

ii) Fafanua mbinu zingine tano zinazobainika kwenye utungo huu.(Alama 5)

 Matumizi ya sentensi fupifupi Tukaangaliana. Naisoma hasa...

 Tashhisi-moyo ukaridhia

 Kuchanganya ndimi - Tukapiga selfie. Tukatifua vumbi la beach na kuondoka.

 Nidaa Kifua nacho ni cha ngao!

 Tashibihi-Macho wastani meupe kama theluji Ngozi yake imepweteka kama jejeta.

 Chuku-Sijakutana na mwanamue kama huyu, pengine kuona kwenye sinema!

b) Thibitisha ukweli wa kauli iliyopigiwa mstari kwenye kifungu hiki ukirejelea hadithi ya Nilitamani (alama 10)

 Tumaini anamwonea gere Nina kwa kuwa na mume aliye na mali na maumbile ya kuvutia- mrefu kiasi, si mweupe si mweusi.

 Utingo anambeba Tumaini bila nauli kutoka Kigamboni hadi Kariokoo

 Cheichei anampa Tumaini shilingi elfu tano za Tanzania na kumpa namba yake ya simu baada ya Tumaini kumrai amsaidie

 Tumaini anapomwona Romeo kwa mara ya kwanza alimtamani. Alimwona kama mwanamume aliyetaka awe naye. Alitamani aolewe naye hata jana.

 Romeo anaonyesha uungwana kwa Tumaini. Anamwongelesha kwa upole pale Coco beach, akamshika mkono kumsimamisha na kumfungulia mlango wa gari.

 Romeo alikuwa na umbile la kuvutia uliomfanya Tumaini anasike na moyo wake kumridhia

 Romeo anampeleka Tumaini kupata chamcha katika migahawa mikubwa

 Romeo anamweleza Tumaini atakavyomfanya awe tajiri.Amiliki baadhi ya mali yake, majumba ya kifahari ya kukodishwa, viwanda vya mafuta vya alizeti na kuanzisha miradi ya burudani kisiwani Zanzibar

 Mpapaso wa Romeo kwa Tumaini unampa msisimkowa aina yake. Alihisi ni kama mizuka inampanda.

 Tumaini alipomwangalia Romeo alipokuwa akimpapasa aliona mara anageuka mweupe, mara mwekundu.

 Tumaini anatambua kuwa Romeo hakuwa mtu wa kawaida, alikuwa jinni

7. Sabina "...Mizizi ya elimu ni michungu ila matunda yake ni matamu. Ikiwa mnataka kuyaonja matunda ya elimu lazima mtie bidii kwani mtaka cha mvunguni sharti ainame..."

a) Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4)

 Ni mameno ya mwalimu mkuu

 Kwenye mawazo/kumbukumbu za Sabina.

 Alikuwa anawazia kuhusu matoke ya mtihani ambao alikuwa anatarajia kuufanya iku ya Jumanne.

 Sabina alikuwa nyumbani kwa Ombati.

b) Tambua mtindo kwenye dondoo hili (alama 4)

 Msemo- mtie bidii

 methali- mtaka cha mvunguni sharti ainame

 Taswira- mizizi ya elimu ni michungu

 Jazanda- Mizizi ya elimu- jitihada za kutafuta elimu

c) Eleza nafasi ya mrejelewa. (alama 6)

Anayerejewa ni Sabina

 Kupitia kwake, sifa ya Yunuke kuwa katili inadhihirishwa. Anamtesa na kumtumikisha Sabina akiwa na umri mdogo.

 Ni kielelezo cha watoto watiifu katika jamii. Anawatii Yunuke na Ombati ingawa wanamtesa.

 Kupitia kwake maudhui ya dhuluma yanabainika. Katika umri wake mdogo anafanya kazi zote za nyumbani na shambani, kuwalisha na kuwakama ng’ombe.

 Anaendeleza ploti. Kupitia kwake tunafahamu matatizo wanayopitia watoto yatima. Alifiwa na mama mzazi, kukataliwa na baba, kufiwa na babu na nyanya.

 Kieleleo cha watu wenye bidii masomoni. Bidii yake inamfanya kuibuka wa saba bora kwenye matokeo ya kitaifa.

 Kupitia mawazo yake, tunapata wahusika kama vile Mwalimu mkuu kuwa mshauri mwema kwa kuwahimiza wanafunzi watie bidii masomoni ili kufanikiwa maishani

d) Tambua toni kwenye dondoo (alama 2)

 Toni ya kuhimiza/ kushauri- mwalimu mkuu anawashauri wanafunzi.

e) Jinsia ya kike imesawiriwa kuwa dhaifu na inazidi kudhulumiwa kila kuchuo. Thibitisha ukweli wa kauli hii ukirejelea hadithi hii (alama 4)

 Sabina anakandamizwa na Yunuke kwa kufanyishwa kazi ote a nyumbani na shambani.

 Mimba za mapema- nyaboke anapata mimba ya Sabina akiwa kidato cha pili

 Kukatiziwa masomo- Nyaboke analazimika kukatiziwa masomo ili kushiriki vibarua muradi amlee Sabina

 Kukataliwa na wanaume- mwanaume aliyemringa mimba Nyaboke alimkana mchana peupe. Analazimika kumlea Sabina peke yake.

 Kutengwa na wanajamii- baada ya kifo cha mamake ksha nyanya na babu, Sabina anatengwa na wanajamii kwa tuhuma za kutoka kwenye familia iliyo na mikosi mingi.

 Elimu ya msichana haithaminiwi- mjomba Ombati hakuthamini elimu ya Nyaboke, alitaka kumwoza Sabina kwa mwendsha pikipiki badala ya kumfadhili katika elimu ya sekondari.

 Ndoa za mapema na za kupangwa- Ombati alipanga kumwoza Sabina kwa mwendesha pikipiki licha ya umri wake mdogo.

 Kupigwa- Yunuke anampiga Sabina vibaya kwa kuchelewa kurudi nyumbani toka shuleni.

 Kutusiwa na kusimangwa- Yunuke anamwita Sabina kiokote asiyekuwa na shukrani.

 Pia anamwita mjalaana na baradhuli mkubwa.

 Kukosa muda wa kusoma- Sabina anafanya kazi nyingi za nyumbani kiasi kwamba hapati muda wa kusoma. Mwalimu mkuu analazimika kuingilia kati kwa kushauriana na mjomba Ombati ili Sabina apewe muda wa kusoma.

8. “Yu wapi kirukanjia wako? Wajua yuko wapi? Uliacha mbachao kwa msala upitao. Atakutunza nani, maana kwako fadhila za punda ni mashuzi!”

a. Yaweke maneno haya katika muktadha wake. (alama 4)

 Ni maneno ya mamake Luka.

 Anamwambia Luka.

 Yumo katika hospitali (Luka).

 Ni baada ya gavana Luka kuhusika kwa ajali na yule kirukanjia wake akakosa kuja kumwona baada ya kumsaliti Lilia alipokuwa gavana

b. Taja mbinu mbili za lugha zilizotumika katika dondoo hili. (alama 2)

 Methali – usiache mbachao kwa msala upitao.

 Swali la balagha – yu wapi kirukanjia wako?

 Takriri - …wapi…wapi

 Nidaa - …mashuzi!2x1=2

c. Bainisha toni ya dondoo. (alama 1)

 Huzuni, Majuto, uchungu

d. Fafanu asifa zozote tatu za mzungumziwa. (alama 3)

 Mwenye bidii.

 Ni laghai.

 Msaliti.

 Mzinzi.

 Ni katili.

 Mnafiki.

 Ni msomi.

 Mwenye dharau.

e. Kwa kurejelea hadithi “Fadhila za Punda” onyesha ukweli wa kauli kuwa fadhila za punda ni mashuzi kwa mifano mwafaka. (alama 10)

 Luka anaachiwa kanisa na pastor Lee Imani baadaye anauza kanisa ili awanie gavana.

 Lilia anampenda Luka na anamshawishi babake akubali kuwabariki lakini Luka anamsaliti Lilia anapokuwa gavana kwa kumpiga makofi na teke la tumbo.

 Luka anamsaliti pastor Lee baada ya kumkubali na kufadhili elimu, baadaye anakuwa na uhusiano na mtoto wake anayemtesa baadaye.

 Luka anawasaliti waumini kwa kuuza kanisa na kuingia siasani.

 Luka anamtendea uovu mkewe anapokosa kuandamana naye kwenye kampeni na kumtusi kuwa amenona kama nguruwe na kwamba wanawake ni wengi.

 Luka anawasaliti wananchi waliomchagua kwa kutotimiza ahadi alizowatolea wakati wa kampeni.

 Luka anamsaliti mkewe kwa kuwa na uhusiano ka kiruka njia.

 Kirukanjia anamsaliti Luka kwa kukosa kumtembelea hospitalini baada ya kujulishwa na daktari huenda asiweze kutembea tena licha ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi naye.

 Lilia anamsaliti babake kwa kuacha kazi ya meneja wa benki baada ya babake kumsomesha na kupata kazi ili awe akipokea wageni wa Luka.

 Lilia anamsaliti babake kwa kushinikiza aolewe na Luka, ingawa babake hakutaka.

 Lee anamsaliti Lilia kwa kumrithisha Luka Kanisa

9. Huku ukirejelea hadithi zifuatazo tano jadili maudhui ya migogoro kwa kutoa mifano maridhawa. (alama 20)

i. Fadhila za punda

Lilia na Luka wana mgogoro unaosababisha vita k.m anapojitazama kwenye kioo anaona kovu shavuni na donda.

 Mapenzi ya Lilia na Luka yanaleta mgogoro kati ya Lilia na babake-hapendi uhusiano ule.

 Kuna mgogoro wa kinafsia kwa babake Lilia anayemshuku Luka kuwa na uhusiano na mwanawe Lilia.

 Luka kumvamia mkewe na kumvuta nywele kumwelekeza kwenye chumba cha kulala, ambapo anampiga ngumi na mateke.

 Luka anamtawisha Lilia na hata kumlazimisha kuandamana naye kwenye kampeni na hii inawafanya wakosane – Luka anamwambia wanawake ni wengi.

ii. Msiba wa kujitakia

 Kati ya viongozi na raia ambao wako tayari kupigania haki zao-hawapewi huduma na viongozi.  Zuhura na Machoka-Zuhura angependa kumchagua kiongozi kwa misingi ya kikabila kinyume na Machoka.

 Sugu Junior na Fumo Matata – Fumo anaona dai la serikali kwamba kuna maendeleo ni porojo tu.

 Mgogoro kati ya tume ya uchaguzi na wananchi.

 Mgogoro wa ushindi wa Sugu Junior dhidi ya Fumo matata.

 Kati yam zee Sugu Senior na Zuzu Matata; ambapo mzee Sugu senior alitwaa uongozi baada ya kuondoka kwa wakoloni.

iii. Mapambazuko ya machweo

 Mzee Makutwa kumtifulia mzee Makucha vumbi na kumdhihaki kuhusiana na kazi yake.

 Bi Macheo anajikuta katika mgogoro na mumewe kwa vile hapendi jinsi mzee Makutwa anavyomfanyia stihizai mumewe.

 Mzee Makucha anakuza mgogoro anapomwitia polisi mzee Makutwa kwa kuwahujumu vijana.

 Mzee Makutwa ana mgogoro na sheria kwa vile anaendesha biashara haramu.

 Migogoro kati ya vijana waliosoma na serikali kwa mfano Sai alidai kuwa vijana wanaachiwa kazi za hadhi ya chini.

 Mzee Makutwa na polisi wakijaribu kumwingiza pangoni.  Mzee Makucha na shirika la reli-kukataa kumlipa pesa.

iv Harubu ya maisha

 Mama Mercy amtaka mumewe aeleze sababu ya kutofika ilhali motto anaelekea kulala. Mama Mercy analalamika kuwa mumewe hatimizi wajibu wake.

 Familia ya Kikwai ina mgogoro na fundi wa nyumba hajalipwa kwa mwezi mzima.

 Kikwai anagongana na Bosi kwa kuacha gari nyumbani kwa kukosa mafuta.

 Nilakosi ana mgogoro wa mpangishaji wake kwa vile hajamlipa na mwezi unaenda kuisha.

 Kikwai kutoleta chakula.

 Kikwai kufika amechelewa.

 Mercy kulalamikia njaa na upweke.

Download this full Document in PDF Now!