MAUDHUI KATIKA CHOZI LA HERI.

Maudhui ni jumla ya mawazo yote yanayozungumzwa pamoja na mtazamo wa mwandishi juu ya mawazo hayo. Hujumuisha mawazo na mafunzo tofauti yaliyomsukuma

USALITI

a)       Polisi wanasaliti wajibu wao wa kulinda usalama kwa kuwaua raia waliokuwa wakipigania mapinduzi

b)      Viongozi wanawasaliti vijana waliowasaidia kupata ushindi kwa kuwasahau baada ya kupata uongozi

c)       Raia wanawasaliti wanawake kama vile mwekevu kwa kuamini kuwa hakushinda kihalali, wanadai aliiba kura na kununua kina mama

d)      Wakweze selume wanamsaliti kwa kudai kuwa alimuunga mkono mwekevu

e)      Mzee kedi anausaliti ujirani aliokuwa nao na familia ya Ridhaa kwa kuwaua familia yake kwa kuwateketeza moto

f)        Wanafunzi wa shule ya Ridhaa wanamsaliti Ridhaa kwa kumtenga kwenye mchezo wao

g)       Mke wa jirani ya Ridhaa anasaliti wageni kwa kulalamikia uuuzaji wa mashamba ya wenyeji kwao

h)      Mkoloni anamsaliti mwafrika kwa kupuuz sera za umiliki wa ardhi na kuamua kujumuisha pamoja ardhi iliyokuwa inamilikiwa na mtu binafsi na kudhinisha umiliki wa hatimiliki

i)        Mpinzani mkuu wa mwekevu anawasaliti raia ya wahafidhina kwa kukataa kukubali matokeo ya uchaguzi jambo linalosababisha maafa na uharibifu wa mali baada ya kuchochea wafuasi wake

 

j)         Mkewe kiriri na wanawe wanamsaliti wanapoenda ngambo na kumwacha kwa upweke na ukiwa uliosababisha kifo chake

k)      Shirika la maghala linawasaliti raia kwa kuwauzia mahindi yaliyoharibika ambayo yalikuwa hatari kwa usalama wao

l)        Mzungu mwenye kahawa anawasaliti wafanyakazi wake anapowanyima bima ya matibabu licha wafanyakazi hao kumsaidia kupata mamilioni ya pesa

m)    Shirika la fanaka linamsaliti Lunga kwa kumfuta kazi kwa kupinga kitendo cha kuwauzia raia mahindi yaliyoharibika

n)      Lunga kiriri anasalitiwa na raia baada ya kufutwa kazi licha lunga kuwatetea wasiuziwe mahindi yaliyoharibika

o)      Naomi anamsaliti mumewe kwa kutoroka na kuacha watoto wake nyuma

p)      Sally anamsaliti billy kwa kumwacha baada ya kufunga ndoa kwa sababu billy alijenga nyumba ambayo haikumpendeza

q)      Sauna anawasaliti wajiri wake kwa kuwaiba watoto na kuwapelekea bi kangara anayewatumia katika madanguro na ulanguzi wa dawa za kulevya

r)        Satua, mke wa jirani ya chandachema analalamikia kila kitu anapohamia kwake mpaka inabidi chandachema kujiondokea. Huo ni usaliti

s)       Mwalimu mkuu anamfukuza zohali kwa sababu ya ujauzito

t)        Subira anaitwa mwizi wa mayai ya kuku wake kwa kuwa ni mbamwezi.

u)      Uongozi unamsaliti shamsi kwa kutompa kazi baada ya kuhitimu. Unamtaka kutoa hongo

v)       Tuama anamsaliti mamake ambaye aliendesha kampeni dhidi ya ukeketaji kwa kujificha na kuketwa

w)      Halmashauri ya elimu inawasaliti wanafunzi wanaotoka katika familia maskini kwa kuwapa mikopo wanafunzi kutoka familia zinazojiweza na kuwaacha wanafunzi maskini wajifanyie vibarua ili kujilipia karo

x)       Mama wa mtoto aliyeokotwa na Neema anamsaliti mtoto huyo kwa kumtupa katika biwi la taka

y)       Bwana Maya anamsaliti mkewe kwa kumwendea kinyume na binti yake Sauna na kumpa ujauzito

NAFASI YA VIJANA KATIKA JAMII

a)       Wana (jinsia zote) Ni wasomi- vijana kama Tila, Umu na Mwaliko walikuwa wenye bidii masomoni.

b)      Walanguzi wa dawa za kulevya — Dick alikuwa akilangua za kulevya kwa muda wa miaka kumi.

c)       Wenye bidi Umu na Dick walikuwa na bidii katika masomo yao.

d)      Wajinga - vijana wengine wa kike walikubali kukeketwa. Wengine waliiaga dunia na wengine kulazwa zahanatini.

e)      Waraibu wa dawa za kulevya- Dick anasema kuwa alikuwa akitumia dowa hizi ili kujirahisishia kazi yoke ya kulangua.

f)        Wapenda fujo vijana ndio waliotumiwa na wanasiasa kuute-keleza uovu wa mauaji na kuyaharibu mali ya wenzao.

 

g)       Katili- kuna vijana waliowabaka mabinti zake Kaizari na kumuumiza mke wake.

h)      Wasio na huruma- vijana wengine walikuwa wakiwaua wenzao bila huruma.

i)        Wasio na msimamo dhabiti- vijana wengine wakipotoshwa na wanasiasa bila kuwaza na kuwazua.

j)         Vijana ni wepesi wa kushawishika-wnansaidia viongozi kupata kura lakini baadaye viongozi hao wanawasahau

k)      Vijana jasiri-wanaendeleza mapinduzi yao licha ya askari kuwaelekezea risasi na vitoza machozi

l)        Vijana wamepevuka kimawwazo-mfano tila

m)    Vijana wamewajibikavijana ambao walitumwa na mashirikanyasiyo ya kiserekali kutoa huduma za ushauri na uelekezi wanwasaidia mwanaheri na lime kwa kuwapa matibabu

NAFASI YA MWANAMKE KATIKA JAMII

Mwanamke amesawiriwa kwa namna mbalimbali:

a)       Mwanamke ni Msomi-Tila alikuwa akimudu masuala ya sheria. Hakuna aliyethubutu kuuchangia mijadala kwani katika masuala ya sheria Tila alikuwa ameyamudu kweli kweli. Selume- Ridhaa alimfariji na kumwomba asilie kwani mwana wake yu hai tena ana kisomo na amehitimu kama mkunga, anaweza kujitegemea. Umulkheri pia alisoma na kuhitimu vizuri.

b)      Mwanomke ni Mjinga- Tuama alikuwa amejipata katika hali mbaya kwa kukubai kupashwa tohara. Alibahatika kwa kuwa hakuiaga dunia kama wenzake. Tuama anaitetea mila hii ya upashaji tohara kwa wanawake eti haijapitwa na wakati kwani bila tohara mwanamke hubakia kuwa mtoto. Huu ni ujinga na upumbavu.

c)       Mwanamke ni mwenye bidii- tunaelezwa kuwa Umulkheri alikuwa nyuma yake Dick akiwa amepiga foleni. Anasafiri ng'ambo kwa shahada yake ya uhandisi katika masuala ya kilimo. Umu, baada ya kuchukuliwa na Mwangeka na Apondi alifanya bidii masomoni na kufuzu vyema katika mitihani yake.

d)      Mwanamke ni mwenye tamaa ya mali- Naomi hakuwekwa na mazingira haya mapya(Mlima wa Simba). Asubuhi moja ' alimtumia Lunga ujumbe na kumtaarifu kuwa ameondoka; akatambe na ulimwengu na huenda akaambulia cha kumsaidia Lunga kuikimu familia. Akawaacha Lunga na wanawe.

e)      Mwanamke ni mwenye huruma- Apondi na Neema walijitwika jukumu la kuwalea wana ambao si wao kwa upendo na imani.

f)        Mwanamke ni katili muuaji- Mamake Sauna aimsaidia Sauna kuavya mimba aliyokuwa amepachikwa na babake mlezi. Neema naye alikuwa ameavya mimba nyingi akiwa kwenye Chuo kikuu.

g)       Mwanamke ni mwenye majuto- Neema aikuwa mwenye kujuta kwa kupoteza nafasi ya kupanga mtoto.

h)      Mwanamke ni mwenye kujiheshimu- Zohai amewahi kupigana na majitu yaiiyokuwo yakitako kuuhujumu utu wake kwa kumnyanyasa kijinsia.

i)        Mwanamke ni mcheshi- Terry ambaye kawaida yake ni mcheshi hakunyamaza bali alimwambia Ridhaa kuwa kwake lazima kila jambo liwe na kiini. (Mwanafunzi aongezee hoja.)

UKATILI

a)       Licha ya kuwa jirani wa Ridhaa kwa miaka mingi, mzee kedi anaiangamiza familia yake kwa sababu hawakuwa wenyeji wa msitu wa heri

b)      Wenyeji wa msitu wa heri wanaeneza vikaratasi vya kuwa mna gharika kwa wasiokuwa wenyeji bada ya kutawazwa kwa kiongozi mpya

c)       Wazungu wanapiga marufuku umilikaji wa ardhi wa waaafrika katika sehemu zilizotoa mazao mengi

d)      Polisi wanawaua mamia ya watu wasio na hatia kwa risasi na mapigo ya rungu

 

e)      Vijana wanayachoma moto magari na kuwapiga watu

f)        Baadhi ya ria wanadhiriki kuingia kwenye maduka ya wafanyi biashara na kupora

g)       Mabarobaro watano wanaoingia kwa kaizari, wanampiga mkewe mpaka anazirai na kuwabaka mabinti zake wawili

h)      Polisi wa “penda usugu ujutewanawarashia raia vijana risasi kwenye vifua na kuwaua

i)        Viongozi wanaahidi vijana kazi lakini wanapopata uongozi wanawasahau

j)        Askari wanawafyatulia risasi na vitoza machozi waandamanaji wanaopinga kuhamishwa kutoka msitu wa mamba na kuwaua

k)       Shirika la maghala ya nafaka linamfuta lunga kwa sababu ya kupinga kitendo cha raia kuuziwa mahindi yaliyoharibika

l)        Mzungu anawanyima wafanyikazi wake bima ya matibabu

m)    Viongozi wa shirika la fanaka wanawauzia raia mahindi yaliyoharibioka licha ya kutahadharishwa kuwa yalikuwa hatari kwa usalama wa binadamu

n)      Naomi anaondoka na kumwachia lunga watoto na uchungu wa moyo ambao unamsababishia mauko

o)      Sauna anatoweka na ndugu zake umu, dick na mwaliko na kumwachia upweke

p)      Sally anamwacha billy baada ya kufunga ndoa naye kwa ajili ya kujenga jumba ambalo halikumvutia na kumwachia maumivu makubwa

q)      Sauna anawaiba watoto na kuwapelekea bibimoja anayewatumia katika madanguro na ulanguzi wa dawa za kulevya

r)       Dick anaingizwa katika biashara haramu ya uuzaji wa dawa za kulevya na buda licha ya umri wake mdogo

s)       Tindi anampeleka lemi kwenye sherehe na kumfungia hadi asubuhi akiendeleza starehe zake

t)        Umati unamchoma lemi kwa kusingizia wizi wa simu ambao hakuwa ametekeleza

 

u)      Bwana maya anamdhalilisha sauna na kumpa ujauzito

v)       Mamake sauna anapokea Makonde, vitisho na matusi anapouliza swali lolote

w)     Mama mtoto aliyeokotwa na Neema anamtupa mwanawe kwenye biwi la taka

x)       Bwana kimbaumbau anampitisha naomi kwenye makuruhu yasiyomithilika yakiwemo kupigwa, kuzingiziwa uwizi, kukatwa mshahara n akumfuta kazi kwa sababu ya kumkataa kimapenzi

UWAJIBIKAJI

a)       Wanaharakati wa kupigania haki za kibinadamu wanaanzisha mradi wa opereshi rudi edeni unaowasaidia Ridhaa na kaizari na familia zao kurudi nyumbani

b)      Kura zinapohesabiwa upya mpinzani wa mwekevu anakubali kushindwa na kutoa wito kwa raia kusahau yaliyopita na kuganga yajayo

c)       Jamii ya kimataifa inaingilia kati na kurejesha amani katika nchi ya wahafidhina

d)      Makaa amekwenda kuwaokoa watu waliokuwa wakipora mafuta kutoka kwenye lori lililobingiria na kusababisha kuchomeka kwake asibakie lolote

e)      Ridhaa anaenda hospitalini kumfanyia upasuaji majeruhi wa maandamano dhidi ya matokeo ya uchaguzi wa wawakilishi wa eneogatuzi

f)        Baada ya kipigo alichopewa babake, Mwangeka anawajibikia masomo yake hadi chuo kikuu alikosomea uhandisi

g)       Ridhaa anawajibika kumtahadharisha Mwangeka dhidi ya kuanza ujenzi kabala ya uchunguzi kufanywa kuhusiana na kiwanja chenyewe

h)      Kangata anatetea ndoa ya bintiye lucia kwenda ukoo wa waombwe waliokuwa maadui sugu wa ukoo wa anyamvua

i)        Kiriri anayadhamini masomo ya mabinti wa kangata licha ya kujua kuwa wao ni nyamvua

j)        Lunga kiriri anawashauri watu wasilime karibu na mito badala yake wachimbe mitaro kuzuia mmomonyokowa udongo

k)      Lunga anapinga kitendo cha raia kuuziwa mahindi ambayo yalikuwa yameharibika

l)        Bi dhahabu anamsajili umu na wengine watano shuleni kwa ushauri wa wizara ya elimu

m)    Bi dhahabu haishi kumhimiza umu kuwa  jasiri katika kukabiliana na hali yake mpya

 

n)      Umu anawajibika kumpa kijana mmoja wa ombaomba pesa alizokuwa ametunduiza kutokana na mapeni aliyokuwa akipewa na babake kama masurufu

o)      Serikali inamuokoa hazina kutokana na kinamasi cha uvutaji gundi na matumizi ya mihadarati na kumpa mafunzo ya upishi yanayomwezesha kupata kazi kama mhudumu katika hoteli

p)      Hazina anamsaidia umu kwa kumnunulia chakula na kumjulisha kwa mama aliyesimamia makao, julida

q)      Julida anampa umu makao ya muda na kumsaidia kupata uhamisho katika  shule ya tangamano

r)       Apondi anawajibika na kuwashauri polisi kutumia ushauru badala ya vipigo kwa raia

s)       Mwangeka na apondi wanawasaidia wahitaji waliomiminika kwao kutoka eneogatuzi lao

t)        Mama aliyekuwa akisimamia makao ambamo umu aliishi kwa ushirikiano wa mwalimu mkuu wa tangamano wanamtafutia umu ufadhili kwa apondi na Mwangeka

u)      Dick anaamua kuachana na biashara haramu na kuanzisha biashara yake ya kuuza vifaa vya umeme wa simu

v)       Apondi na Mwangeka wanakubali kumchukua umu kama mtoto wao wa kupanga

w)     Babake Tuama anaendeleza kampeni dhidi ya ukeketaji wa wasichana kijijini

x)       Nyanyake pete anamtetea dhidi ya kuozwa kwa mzee fungo akiwa mtoto mdogo

y)       Pete anahangaika kwenye vibarua vya mshahara mdogo ili kumkimu mwanawe

TAMAA NA UBINAFSI

a)       Vinara wa taasisi mbalimbali za umma wananyakua ardhi ya msitu na kuwaacha wanyama bila makao

b)      Viongozi wa shirika la maghala ya fanaka wanawauzia raia mahindi yaliyoharibika kwa sababu ya tamaa

c)       Baadhi ya viongozi wanayakua hata madhabahu kwenye mlima wa nasibu ili kujenga hoteli za kitalii

d)      Mkewe kiriri, annete na wanawe wanaenda ughaibuni na kumwacha kiriri kwenye upweke na ukiwa unaosababisha kifo chake

e)      Sauna anaongozwa na tamaa ya kutajirika hivyo anajihusisha na kuwaiba watoto

f)        Bi kangara kwa sababu ya tamaa ya pesa analangua watoto wanaotumika katika madanguro na ulanguzi wa dawa za kulevya

g)       Baada ya kutangazia raia kuwa msitu wa mamba ni marufuku, viongozi wanaendeleza ukataji miti na uchomaji wa makaa usiku

 

h)      Umu anawajibika kumpa kijana mmoja wa ombaomba pesa alizokuwa ametunduiza kutokana na mapeni aliyokuwa akipewa na babake kama masurufu

i)        Serikali inamuokoa hazina kutokana na kinamasi cha uvutaji gundi na matumizi ya mihadarati na kumpa mafunzo ya upishi yanayomwezesha kupata kazi kama mhudumu katika hoteli

j)        Hazina anamsaidia umu kwa kumnunulia chakula na kumjulisha kwa mama aliyesimamia makao, julida

k)       Julida anampa umu makao ya muda na kumsaidia kupata uhamisho katika  shule ya tangamano

l)        Apondi anawajibika na kuwashauri polisi kutumia ushauru badala ya vipigo kwa raia

m)    Mwangeka na apondi wanawasaidia wahitaji waliomiminika kwao kutoka eneogatuzi lao

n)      Mama aliyekuwa akisimamia makao ambamo umu aliishi kwa ushirikiano wa mwalimu mkuu wa tangamano wanamtafutia umu ufadhili kwa apondi na Mwangeka

o)      Dick anaamua kuachana na biashara haramu na kuanzisha biashara yake ya kuuza vifaa vya umeme wa simu

p)      Apondi na Mwangeka wanakubali kumchukua umu kama mtoto wao wa kupanga

q)      Babake Tuama anaendeleza kampeni dhidi ya ukeketaji wa wasichana kijijini

r)       Nyanyake pete anamtetea dhidi ya kuozwa kwa mzee fungo akiwa mtoto mdogo

s)       Pete anahangaika kwenye vibarua vya mshahara mdogo ili kumkimu mwanawe

TAMAA NA UBINAFSI

a)       Vinara wa taasisi mbalimbali za umma wananyakua ardhi ya msitu na kuwaacha wanyama bila makao

b)      Viongozi wa shirika la maghala ya fanaka wanawauzia raia mahindi yaliyoharibika kwa sababu ya tamaa

c)       Baadhi ya viongozi wanayakua hata madhabahu kwenye mlima wa nasibu ili kujenga hoteli za kitalii

d)      Mkewe kiriri, annete na wanawe wanaenda ughaibuni na kumwacha kiriri kwenye upweke na ukiwa unaosababisha kifo chake

e)      Sauna anaongozwa na tamaa ya kutajirika hivyo anajihusisha na kuwaiba watoto

f)        Bi kangara kwa sababu ya tamaa ya pesa analangua watoto wanaotumika katika madanguro na ulanguzi wa dawa za kulevya

g)       Baada ya kutangazia raia kuwa msitu wa mamba ni marufuku, viongozi wanaendeleza ukataji miti na uchomaji wa makaa usiku

 

h)      Tamaa na anasa inamfanya tindi kumfungia lemi ili aweze kuendelea na anasa zake

i)        Tamaa ya mali inamfanya buda kumwingiza dick katika biashara haramu akiwa na umri mdogo

j)        Tamaa ya pesa inawafanya walinda usalama kupokea hongo n akumruhusu buda kuendeleza biashara yake haramu ya uuzaji wa dawa za kulevya

k)       Tamaa ya pesa inafanya maafisa wa forodha kupokea hongo na kumruhusu dick kupitisha dawa za kulevya zinazoenda kuuzwa ngambo

l)        Tamaa ya kupanga ya mtoto inawafanya mwangemi na Neema kumpata mwaliko kutoka kituo cha benefactor

m)    Tamaa za kimwili zinamfanya zinamtuma bwana maya kumdhalilisha sauna katika chumba chake na kumpa ujauzito

UTU

a)       Bi dhahabu anamsajili umu na wengine watano shuleni kwa ushauri wa wizara ya elimu

b)      Bi dhahabu haishi kumhimiza umu kuwa jasiri katika kukabiliana na hali yake mpya

c)       Umu anawajibika kumpa kijana mmoja wa ombaomba pesa alizokuwa ametunduiza kutokana na mapeni aliyokuwa akipewa na babake kama masurufu

d)      Mwangeka na Apondi wanawasaidia wahitaji waliomiminika kwao kutoka eneogatuzi lao

e)      Mama aliyekuwa akisimamia makao ambamo umu aliishi kwa ushirikiano wa mwalimu mkuu wa tangamano wanamtafutia umu ufadhili kwa apondi na Mwangeka

f)        Apondi na Mwangeka wanakubali kumchukua umu kama mtoto wao wa kupanga

g)       Serikali inamuokoa Hazina kutokana na kinamasi cha uvutaji gundi na matumizi ya mihadarati na kumpa mafunzo ya upishi yanayomwezesha kupata kazi kama mhudumu katika hoteli

h)      Hazina anamsaidia umu kwa kumnunulia chakula na kumjulisha kwa mama aliyesimamia makao, julida

i)        Julida anampa umu makao ya muda na kumsaidia kupata uhamisho katika shule ya tangamano

UKOSEFU WA UWAJIBIKAJI

a)       Uongozi hauleti ahueni yoyote katika maisha ya raia

b)      Nyanyake mwanaheri anamwona subira kuwa chanzo cha kuharibiwa kwa amali yao

c)       Wazazi wa zohali wanamtelekeza kwa sababu ya kuwa na ujauzito

d)      Mwalimu mkuu anamfukuza zohali shuleni kwa sababu ya kuwa na mimba

e)      Fumba anamwendea kinyume mwanafunzi wake, Rehema na kumpa mimba ya chandachema.

f)        Bwana tenge anafanya ukware mbele ya wanawe wakati mkewe, bi. Kimai anapokwenda mashambani

g)       Polisi wanatatua mizozo midogomidogo kwa makeke na bunduki

 

h)      Kulingana na apondi baadhi ya polisi wanashirikiana na wahalifu kutekeleza wizi na kugawana ngawira

i)        Baadhi ya polisi pia kulingana na hotuba ya apondi wanayaacha magari makuukuu barabarani kwa sababu wenye ma y8hegfgari haya ni miamba isiyogusika

j)        Uongozi haumpi shamsi kazi baada ya kuhitimu, unamtaka atoe hongo

k)       Babake pete anamkataa kwa kuw alizaliwa nje ya ndoa jambo linalomsababishia dhiki kubwa maishani

l)        Mamake pete hashughulikii mahitaji ya pete hata kumnunulia sare

m)    Wajomba wa pete wanamwoza pete kwa mzee fungo kama mke  wanne akiwa darasa la saba

n)      Pete anakosa kuwajibika anapojaribu kuavya mimba mara mbili

UKABILA

Ukabila ni matendo au fikira za mtu za kuthamini kabila lake mwenyewe tu na kuwabagua wa makabila mengine.

a)       Ukabila umejitokeza kama ifuatavyo katika Chozi la Heri. Subira alitengwa na familia ya mume wake kwa kuwa wa kabila tofauti na lao. Mwanaheri anatueleza kuwa mama yake alikuwa ametoka kwenye jamii ya Mamwezi lakini babake alikuwa wa jamiii tofauti. Kila mara Subira aliitwa 'muki' au huyo wa kuja. Kwa miaka mingi aliweza kuvumilia kubaguliwa, kufitiniwa na kulaumiwa kwa asiyoyatenda. Mwishowe alihiari kujiondokea na kwenda mjini alikojinywea kinywaji kikali, akafaia alitengwa katika michezo yao.

b)      Kijana mmoja alimwita 'mfuata myua' jambo lililomuumiza sana Ridhaa.

c)       Mzee Kedi alimtendea udhalimu Ridhaa na kuiteketeza aila yoke licha ya wao kuwa majirani kwa miaka hamsini. Ridhaa alifanyiwa hivi kwa kuwa alikuwa ametoka kwenye kabila tofauti na Kedi.

d)      Ami zake Kangata walimsuta mno kwa kumwoza mwanawao kwa mtu wa jamii tofauti na yao. Walishangaa ni vipi mwana wao ataozwa kwa mtu wa ukoo ambao huvaa nguo ndani nje. Waliamini kuwa ukoo huo huzaa majoka ambao hata kiporo cha juzi hayawezi kukupa.

e)      Ndoa ya Selume iisambaratika baada ya Vita vya kutawazwa kwa kiongozi mpya. Alibaki mwenye kilio baada ya wambea kumfikishia ujumbe kuwa mume wake amekwisha kuoa msichana wa kikwao.

f)        Tulia alimsaidia Kaizari kufunganya na kumsindikiza hadi njia panda. Alimkumbatia na kumwambia kuwa mwenyezi Mungu ndiye hupanga na nguvu na mamlaka pia hutoka kwake. Akamjuvya kuwa uongozi mpya umezua uhasama kati ya koo ambazo zimeishi kwa amani kwa karibu karne moja.

g)       Nyanyake mwanaheri anamlaumu subira, mamake kuwa ndiye aliyekuwa chanzo cha majirani kuwachomea boma kwa sababu ya kutoka jamii ya bamwezi

 

UKIUKAJI WA HAKI ZA WATOTO

h)      Dick anaingizwa katika biashara haramu licha ya umri wake mdogo

i)        Buda anamtisha dick kuwa atamtupa nje na kumsingizia wizi na kuchomwawakati anapokataa kushiriki katika biashara haramu

j)        Dadake lemin anampeleka kwenye sherehe n akumfungia hadi asubuhi akiendeleza starehe zake

k)       Umati unamchoma lemi kwa kusingiziwa uwizi wa simu ambao hakuwa ametekeleza

l)        Tindi anatoroka na kumwacha lemi kuchomwa kwa kisingizio cha wizi wa rununu

m)    bwana maya anamdhalilisha sauna katika chumba chake na kumpa ujauzito

n)      mamake sauna anamshurutisha sauna kuavya mimba ya babake

o)      mama mtoto aliyeokotwa na Neema anamtupa mwanawwe kwenye bili la taka

ATHARI ZA MATUMIZI YA MIHADARATI

a)              Zohali anajiunga na kundi la vijana na kuvuta gundi inayomfanya kusahau matatizo anayopitia bila kujua mathara yake

b)             Pete anahamia kwa kazi ya kuuza pombe inayosababisha kupata watoto ambao anashindwa  kuwalea na kutaka kujiua

c)              Dick anaingizwa na Sauna katika ulanguzi wa dawa za kulevya zinazohatarisha maisha ya muuzaji anaweza kamatwa na polisi na kufungwa

d)             Dick anashurutishwa kumeza dawa za kulevya na kasha akifika ughaibuni asitapike kutokana na uangalizi mkali katika viwanja vya ndege

e)             Dawa za kulevya zinasababisha vifo kijana msomi anakufa katika hospitali ya mwanzo mpya kutokana na utumiaji wa dawa za kulevya

f)               Shamsi anawapigia kelele majirani wake katika mji wa Ahueni kutokana na ulevi wake

g)              Aidha ulevi unamfanya aishi katika mtaa wa makabwela wa Kazikeni

h)             Kapanga ananusurika kifo kwa matumizi ya kangara inayosababisha vifo vya watu sabini uk143

 

 

MABADILIKO

Hii ni hali ambapo mambo yanaenda kinyume na jinsi yalivyokuwa yakienda mbeleni. Hali ya kufanya mambo kubadilika na kuwa tofauti ya kawaida yake.

a)      Katika ukurasa uo huo wa 11 tunasoma kuwa ridhaa alileta mabadiliko katika msitu wa heri ambao ulikuwa hapo awali umekauka sana lakini baada ya maji ya mabomba kufikishiwa watu kunakuwa na mababadiliko na ile hali ya kuwa jangwa ikaisha, miti mingi ikapandwa na hata mvua nyingi kunyesha.

b)     Maisha ya Ridhaa pia yanachukua mkondo mpya au kubadilika wakati familia yake inapoangamia kwenye janga la moto, na mali yake yote kuishia hapo. Maisha yaliyokuwa ya furaha pamoja na familia yake yanabadilika na kuwa uchungu mtupu na kilio cha kufiwa na wapenzi wake.

c)      Katika ukurasa wa 63-kuna mabadiliko yanayoendelea katika msitu wa Mamba. Tunaambiwa kuwa msitu huu uligeuka na kuwa nyumbani mwa maelfu ya watu waliogura makwao bila tumaini ya kurudi. Maduka na majumba yanajengwa, na ile hali ya kuwa msitu inabadilika, na mashamba ya watu ndiyo yanayoonekana kwa sasa.

d)     Wakimbizi walilazimishwa kutumia misala ya sandarusi na vichaka kinyume na maisha yao ya hapo awali

e)     Mabadiliko ya wanawake kukubaliwa na kuwa viongozi katika jamii mfano mwekevu

f)       Upashaji tohara kupigwa marufuku

g)      Umilikaji wa wa mashamba ulibadiliki kutoka umilikaji wa kijamii hadi ule wa kibinafsi

h)     Maisha ya Naomi yalibadilika baada ya kuondoka kwake na baada ya kuhamia mlima wa simba

i)       Maisha ya Dick yalibadilika baada ya kuacha biashara ya ulanguzi wa dawa za kulevya

j)       Kifo cha Lunga Kiriri kilibadilisha mkondo wa maisha wa watoto wake

k)     Maisha ya Zohali yalibadilka alipopata mimba

l)        Katika ukurasa wa 84, Maisha ya Umu yalichukua mkondo mpya. Siku ile baada ya kuwapigia polisi ripoti, ilibainika kuwa wanuna wake walikuwa wametekwa nyara na Sauna

m)   Katika ukurasa wa 10-Tunapata kuwa mfumo uliokuwepo hapo awali wa kumiliki mashamba barani Afrika ulipigwa marufuku na kukawa na mfumo mpya wa umiliki wa mashamba uliohusisha kupewa kwa hati miliki. Haya ni mabadiliko yanayokuja katika jamii.

n)     Katika ukurasa wa 11-Kuna mabadiliko yanayofanyika katika shule baada ya mamake Ridhaa kuzungumza na mwalimu wake kuhusu umuhimu wa kuwajuza wanafunzi ushirikiano na kuishi kwa umoja. Mabadiliko haya yanakuwa ya maana sana kwa Ridhaa kwani elimu yake inaendelea kwa ufasaha na anahitimu hadi chuo kikuu.

 

o)      Pia katika ukurasa wa 148 tunasoma; “Maisha yangu yalichukua mkondo mwingine nilipojiunga na darasa la saba. Katika jamii yangu, inaaminika kuwa msichana akishaisha kupashwa tohara, ameingia utu uzimani, hivyo ataipaka familia yake tope ikiwa ataendelea kuozea kwao bila mume “

p)      Ridhaa anabadilika na kuanza kutangamana na watu wa kawaida waliolowea kwenye msitu wa mamba licha ya kwamba awali amekuwa akiishi maisha ya kifahari kwenye kasri uk 35

q)      Kuolewa kwa lucia katika ukoo wa waombwe kuliyeyusha chuki baina za koo za waombwe na anyamvua, wakaanza kuweka mbali tofauti zao za awali uk 67

r)       Lunga mtetezi wa mazingira anabadilika na kuwa mhasimu wa mazingira na kuanza kuyaharibu kwa kukata miti na kupanda mimea uk74

s)       Hazina ambaye alikuwa ombaomba mitaani kwa sasa amebadilika akapata elimu na kuajiriwa kuwa mhudumu katika hoteli

MIGOGORO

Migogoro hali ya kuwepo kwa mivutano na mikinzano mbalimbali baina ya wahusika katika kazi ya fasihi. Migogoro huweza kuwa kati ya wahusika, familia zao, matabaka tofauti, nyadhifa mbalimbali, kiuchumi, nafasi katika jamii au hata kisiasa. Aina za migogoro katika riwaya hii.

a)       Kuna mgogoro kwenye familia ya Mzee Mwimo Msubili, kwa sababu familia yake ilikuwa kubwa na hakuitosheleza kwa chakula. Uk 9

b)      Mgonjwa mmoja kwenye hospitali ya mwanzo mpya anapata majeraha mabaya baada ya kuvamiwa na kuumizwa kwenye mzozo wa ardhi katika eneo la Tamuchungu

c)       Panashuhudiwa mgogoro kati ya mzee kedi na familia ya ridhaa pale mzee kedi anaposhiriki katika mauaji ya watu wa aila ya ridhaa uk 3

d)      Panatokea mgogoro kati ya baba na mama ya pete uk 147

e)      Mgogoro wa kijamii unajitokeza baada ya mkoloni kupuuza sera za Mwafrika. Uk 10,”Hatua ya mkoloni ya kupuuza sera za Mwafrika za umiliki wa ardhi na kuamua kujumuisha pamoja ardhi iliyomilikiwa na mtu binafsi na kuuidhinisha umiliki huu kwa hatimiliki, ilivuruga mshikamano wa kijamii “

f)        Kulijitokeza mgogoro shuleni wakati Ridhaa aliitwa ‘mfuata mvua’,na kutengwa na wenzake. Walimwona kama mwizi. Uk 10,”Wewe ni mfuata mvua. Hatutaki kucheza nawe. Umekuja hapa kutushinda katika mitihani yote. Wewe ndiwe unayetuibia kalamu zetu “

g)       Mwekevu ambaye ni mgombea wa kike anapopanda jukwaa kuuza sera zake ili kuwashawishi wampigie kura, wanaume wanamrushia cheche za matusi ila anayastahimili uk 18, huu ni mgogoro wa kijinsia

h)      Ridhaa alijipata katika hali ya mgogoro na nafsi yake. Uk 12,” Miguu yake sasa ilianza kulalamika pole pole parafujo za mwili wake zililegea, akaketi juu ya ya wapenzi wake. Baada ya muda wa mvutano, wa hisla na mawazo, usingizi ulimwiba.

i)        Kulikuwa na mgogoro uliosababishwa na wanasiasa, juu ya nani atakaye kuwa kiongozi wa jamii, kati ya mwanamke mwananume. Uk 19,” MijadaIa hii ilizua na kukuza migogoro isiyomithilika “

j)        Mgogoro mwingine ulijitokeza kati ya raia na wanapolisi, wakiwa katika harakati zao za kuweka amani. Uk 19,” Mchezo wa polisi kukimbizana na raia ulianza katika mchezo huo mamia ya roho zisizo na hatia zilisalimu amri chini ya pambaja za risasi na mapigo ya rungu, vitoa machozi navyo vikafanya kazi barabara.

k)      Nyamvula anajikuta katika mgogoro wa nafsi yake, wakati ambapo imani yake inakinzana na kazi ya kuwa askari. Uk 62,” Kulingana na Nyamvula, kuwa askari wa vita kulikinzana na imani yake, hasa kwa vile Nyamvula alisema ni born again. Mwangeka alimsisitizia kuwa kulinda usalama si sawa na kuua”

l)     Katika ukurasa wa 38 Tila anaitaja migogoro kadha katika Tamthilia ya Hussein. Tamthilia hii ya Mashetani ninayorejelewa ina migogoro mingi sana kama: migogoro ya kisiasa, kiuchumi, na pia ya kijamii.

 

AJIRA

Ni hali ya mtu kuw anakazi amabyo inakuwa ndiyo chemichemi ya mapato ya kuyakimu mahitaji yake

a)       Annete mkewe kangata anapata kazi ya uhazili mwandamizi katika afisi za umma uk 64

b)      Baada ya kuhitimu masomo yake, ridhaa anapata kazi ya udaktari uk 10

c)       Mwangeka anapata fursa ya kwenda nchi za mashariki ya kati akiwa na wadhifa kwenye jeshi, wenye jukumu la kulinda usalama

d)      Kijana aliyevalia shati lililoandikwa ‘hitman’ mgongoni analalamikia ukosefu wa nafasi za kazi, kwamba baada ya kuhitimu, mtu analazimika kupiga lami kwa muda Zaidi ya miaka kumi uk 21

e)      Katika mazungumzo kati ya tila na ridhaa, tila analalamikia ukosefu wa nafasi za kazi kwa vijana unaochochewa na kukithiri kwa ufisadi uk 42

f)        Hazina baada ya kupata elimu uchwara anaajiriwa kama mhudumu katika hoteli uk 88

g)       Baba ya zohali anapatya ajira na kufanya kazi kwa wadhifa wa mkurugenzi katika shirika la utoaji huduma za simu uk98

h)      Rachel Apondi, anafanya kazi katika wizara ya vijana na masuala ya kijinsia

i)        Selume anajiriwa kama muuguzi mkuu katika hospitali ya matibabu ya mwanzo mpya

j)        Kaizari anaajiriwa kama afisa wa matibabu katika hospitali ya matibabu ya mwanzo mpya

NDOA

Ndoa ni maelewano au maafikiano rasmi kati ya mwanamume na mwanamke yanayowawezesha kuishi pamoja kama mume na mke .

a)      Kuna ndoa kati ya Ridhaa na Terry. akamgeukia mumewe tena na kusema, …laiti Ridhaa angalijua kwamba hii ndiyo mara yake ya mwisho kuzungumza na mpenzi mkewe. Tunapata kuwa Ridhaa ana mwoa Terry, uk ll “Baadaye aliamua kuasi ukapera, akapata mke, Terry “

b)     Mwangeka alikuta na Lily Nyamvula katika Chuo kikuu na kumwoa. Walibarikiwa na mtoto mmoja kwa jina Becky. Ndoa hii haikudumu kwani Lily na Becky waliangamia kwenye janga la moto.

c)      Baada ya ndoa ya mwanzo kusambaratika, Mwangeka alimwoa Apondi. Walibarikiwa na mwana wa kiume kwa jina Ridhaa.

d)     Mwangemi alimwoa mwanamke kwa jina Neema. Hawakufaulu kupata mwana wao kindakindaki japo walipanga mwana wao kwa jina Mwaliko.

e)     Kangata alikuwa na mke wake kwa jina Ndarine. Walibarikiwa na wana wafuatao. Lunga Kiriri, Lucia Kiriri na Akelo Kiriri.

f)       Lucia Kiriri — Kangata-,-alikuwa ameolewa katika ukoo wa Waombwe ambao awali walikuwa maadui sugu wa ukoo wa Anyamvua. Ndoa hii ilipata pingamizi sana kutoka kwa ukoo mzima lakini kutokana na Msimamo imara wa Kangata ndoa hii ilisimama. Watu wa ukoo wa kina Kangata walishangaa ni kwa nini mwana wao akaozwa kwa watu ambao huvaa nguo ndani nje na pia huzaa majoka ya mdimu ambayo ni machoyo kupindukia.

g)      Kaizari alikuwa na mke kwa jina Subira. Walibarikawa na mabinti wawili, Lime na Mwanaheri.

h)     Lunga alikuwa na mke kwa jina Naomi. Walikuwa na wana watatu, Umu, Dick na Mwaliko. Ndoa hii haikudumu kwani Naomi alimwacha Lunga na kwenda mjini alikokuwa shangingi kwelikweli.

i)       Pete na Fungo- tunaelezwa kuwa Pete alipoingia darasa Ia saba alipashwa tohara nao wajombake wakapokea posa na baadaye mahari kutoka kwa buda mmoja kwa jina Fungo aliyemuoa kama bibi wa nne. Ndoa hii haikudumu kwani Pete alihiari kumwacha baba huyu.

 

k)      Kuna ndo a kati ya bwana tenge na mke wake bi kimai. Wamejaliwa kupata watoto watano ambao wanaoishi nao katika mashamba ya michai uk 106. Hakuna uamninifu katika ndoa hii kwani bwana tenge anawaleta wanawake wengine mkewe anaposafiri mashambani

l)     Awali kulikuwa na ndoa kati ya mandu na apondi. Mandu aliaga dunia alipokuwa akilinda usalama

UKARIMU

Ni tendo la kuwasaidia watu wenye mahitaji mbalimbali bila masharti

a)       Ridhaa anatumia uwezo wake kuwavutia wanakijiji maji ya mabomba ili yawapunguizie makali ya ukosefu wa maji uk 11

b)      Shirika la makazi bora linajitolea kuwajengea wakimbizi wa msitu wa mamba makazi ma kuwapa vyakula na maji uk 11

c)       Ridhaa aliwasaidia watu mbalimbali kutokana na matatizo mengi waliyokuwa wakiyashuhudia uk 35

d)      Mashirika yasiyo ya kiserikali yanawatuma wawakilishi wao ili kuwapa ushauri na nasaha waathiriwa wa makabiliano yaliyowaishia kulowea msitumi uk 36

e)      Julida anamkaribisha umu kwa furaha na kumhakikishia kwamba atakuwa salama hadi wakati atakapokabidhiwa kwa idara ya watoto uk 189

f)        Marafiki wapya wa umu shuleni wanamhimiza kwa ukarimu avumilie maisha ya shule mpya, kwani siku moja atayazoea uk 91

g)       Mtawa pacha anawonyesha zohali ukarimu kwa kumuokoa kutoka njia ya uharibifu uk 99

h)      Mwalimu mkuu Bi Tamasha wa shule ya msingi wa kilimo anasikiliza kwa makini na ukarimu mkuu masaibu ya chandachema na hatimaye kumsaidia uk 105

i)        Chandachema anaokolewa na shirika la hakikisho la haki na utulivu uk 107

j)        Mwangeka na apondi wanakuwa wakarimu kwa watu wenye mahitaji mbalimbali uk 116

k)      Apondi na mwangeka wanakubali kumchukua umu kama mtoto wao wakiwa radhi kumtunza uk 117

l)        Neema na mwangemi wanakuwa wakarimu wanapokubali kumchukua mwaliko kama mtoto wao wa kupanga

MAUTI/KIFO

Hii ni hali ya mtu au kiumbe chenye kuiaga dunia/kutokwa na uhai. Wahusika wengine wanakutana na janga hili la mauti.

a)       Kangata na Ndarine waliiaga dunia- mwandishi anatujuvya kuwa kwa sasa, miaka mitano imepita na Kangata na Ndarine wameipa dunia kisogo.

b)      Terry na wanawe walikumbana na janga hili la kifo baada ya kuchomwa wakiwa ndani ya nyumba yao.

c)       Mamake Ridhaa aliaga dunia. “Maneno marehemu mamake kuwa mwanamume hufumbika hisia na kuwa machozi ya mwanamume hayapaswi kuonekana hata mbele ya majabali ya maisha.”

d)      Kiriri alikumbwa na mauti- mwandishi ametueleza kuwa Kiriri aliiaga dunia muda mfupi kutokana na kihoro cha kufilisikavna ukiwa aliokuwa ameachiwa na mkewe Annette na wanawe. Subira alikumbana na mauti baada ya Subira kuondoka nyumbani alienda mjini Kisuka na baada ya miezi kadha mumewe alimpata kwenye chumba chake akiwa amejifia.

e)      Nduguye Mwangeka(dede) alikumbana na mauti. Mwangeka anapomkumbuka Tila anatabasamu kisha tone moto la chozi linamdondoka.

f)        Baada ya Lunga kuachwa na mkewe aliiaga dunia mwandishi dhuho wa mwaka alifariki na kuwaacha watoto wake na mikononi mwa wao.

g)       Vijana waliofyatuliwa risasi waliiaga dunia tumeelezwa walimiminiwa risasi vifuani mwao na wote wakaiaga dunia kifo cha kishujaa kwani walijitolea mhanga kupigania uhuru tatu.

h)      Lily Nyamvula na mwanawe Becky waliiaga dunia- Mwangeka ameketi mkabala mwa kidimbwi cha kuogelea nje ya jumba lake la kifahari ambalo yeye aliliona kama makavazi ya kumtonesho donda lililosababishwo na kifo cha mke wake Lily Nyamvula.

i)        Mgonjwa mmoja aliyejifia ni kijana anayesomea shahada ya uzamili, aiikuwa mwathiriwa wa pombe haramu. Wasichana waliokeketwa waliaga dunia.

j)        Mgonjwa kwa jina Tuama alibahatika kwa kuwa hakuiaga dunia kama wenzake waliokuwa wamepashwa tohara kama yeye. Baadhi ya wasichana wanapoteza maisha yao baada ya kupashwa tohara ya wanawake katika jamii ya kina tuama

Tunaeezwa kuwa miezi mitatu baadaye ami yake Mwangeka aliyeitwa Makaa alichomeka asibakie chochote alipokuwa akiwaokoa watu ambao walikuwa wakipora mafuta kutoka kwenye lori lililokuwa

   limebingiria.

k)                   Watu kadhaa wanaangamia katika ajali ya moto uliosababishwa na hitilafu za umeme uk 54 baada ya zima moto kuchelewa kufika

l)          Lemi kakake tindi anaangamia baada ya umati wenye hasira kumwagia petrol na kumteketeza kwa tuhuma za kuiba simu

m)      Kunatokea kifo cha mandu, ambaye alikuwa mumewe apondi, alifariki katika harakati za kulinda usalama uk 115

n)        Ndugu mdogo wa kairu anafariki dunia kutokana na ukosefu wa chakula na maji wanapokuwa safarini wakihamia eneo salama uk 91

o)        Mamake mwanaheri(subira) anafariki dunia baada ya kunywa sumu kufuatia kukatiliwa na familia ya mumewe

p)        Chandachema anatoa taarifa kuhusu kifo cha nyanya yake ambaye alikuwa ndiye mlezi wake baada ya wazazi wake kumtelekeza uk 102

UPWEKE. /UKIWA

Ni hali ya kutokuwa karibu na mtu au watu wa kuzungumza ama kushirikiana nao katika shughuli za kimaisha

a)       Ridhaa anahisi upweke anapowakumbuka aila yake amabao wote waliangamia katika mkasa wa moto uk 5

b)      Mwangeka anajisikia mpweke baada ya kurejea nyumbani kwa vile watu wa aila yake wakiwemo mkewe waliangamia katika mkasa wa moto uk 51

c)       Umu anapoamka asubuhi na kuwakosa ndugu zake dichnan mwaliko, anakumbwa na upweke

d)      Baada ya kutoroka kwa mkewe lunga kiriri anahisi upweke na huzuni hadi akaaga dunia

e)      Kiriri baada ya kuachwa na familia yake walipohamia ng’ambo anahisi upweke, jambo hili linakuja kumwangamiza baadaye

MAJUTO

Majuto ni masikitiko anayokuwa nayo mtu kutokana na makosa aliyoyafanya

a)    Ridhaa anajutia maisha yake ya kale wakati aliposhabikia ukoloni na kushiriki katika ukandamaizaji wa wenzake uk 8

b)   Mwangeka anajutia hatua yake ya kutomsikiliza mkewe alipopinga kazi yake ya kuwa mwanamaji. Anaona kutokuwepo kwake nyumbani kama kiini cha kifo chake

c)    Babake mwanaheri anajutia hatuq ayake ya kutengana na mkewe kwa msingi ya tofauti za kikabila uk 96

d)   Babake zohali baada ya kugundua kwamba zohali ametoroka, anaanza kujutia kwa hatua ya kumtelekeza bintiye hivi hivi kwa sababu ya mimba tu…. uk 101

e)    Neema anajutia kwa nini hakupanga mtoto yule aliyemwokota pipani uk 163

f)     Naomi anajutia hatua ya kuwaacha familia yake uk 192

CHUKI

Ni hali ya kutokuwepo kwa upendo baina ya watu

a)       Ridhaa akiwa mdogo anachukiwa na wanafunzi wenzake shuleni uk 10

b)      Wenyeji wa msitu wa heri wanachukia uwepo wa ridhaa, wanasema uwepo wake utawavurugia Amani na utulivu ambao wamekuwa nao pahali hapo uk 9

c)       Wanafunzi wanasingizia ridhaa kuwa mwizi wa kuwaibia kalamu darasani uk 10

d)      Majirani wa ridhaa akiwemo mzee kedi wanamwonyesha chuki wanapoanza kusambaza karatasi za chuki zinazowataka wahame pahali pale uk 12

e)      Wakimbizi wa msitu wa mamba wana chuki dhidi ya sakari. Wanawarushia askari makombora ya matusi askari wabapojaribu kuwatuliza ili wapewe msaada kwa mpangilio

f)        Jamii zinazoishi kwenye msitu wa mamba wanaanza kuchukiana na hili inawatia tumbo joto viongozi ambao wanaanzisha kampeni za upatanisho uk 75

 

ATHARI YA VITA KATIKA NCHI YA WAFIDHINA 

a)       watu kuuawa, kuacha makwao na kukimbilia maisha yao huku kupoteza mali kwani waliokimbia makwao kila walichokiacha kiliteketezwa

b)      kupora maduka ya Kihindi, kiarabu na hata Waafrika wenzao

c)       Misafara ya wakimbizi ikawa kwenye barabara na vichochoro vya Wahafidhina

d)      Mizoga ya watu na wanyama

e)      magofu ya majumba yaliyoteketezwa kwa moto

f)        uharibifu wa mali na mazingira.

g)       Nyimbo za uchochezi mpinzani wa Mwekevu anambiwa tawala wahafidhina, mwanzi wetu tawala.

h)      Kuchomwa kwa magari kana kwamba ni mabiwi ya taka

i)        Vilio kwa waliokuwa wakiteketezwa

j)        Kubakwa kwa mabinti wa Kaizari yaani Lemi na Mwanaheri

k)      Askari wa fanya fujo uone kuwafyatulia risasi vijana walioamua kufa kishujaa.

l)        Magonjwa ya homa ya matumbo

m)    Njaa na ukosefu wa maji safi

n)      Kukimbilia chakula kwa watu wazima jinsi wafanyavyo watoto

UMUHIMU WA MASHIRIKA YA MISAADA

a)       Mashirika ya kidini yanaungana pamoja kuwasaidia waathiriwa kwa kuwapa chakula katika kambi mbalimbali

b)      Kituo cha Benefactor kimeokoa maisha ya watoto wengi k.m Mwaliko, Mtoto aliyeokolewa na Neema na watoto wengine

c)       Shirika la jeshi la wajane la Wakristu linasaidia maisha ya mayatima kama vile Chandachema, Umu na Mwanaheri uk95

d)      Shuleni tangamano iliwasaidia wanafunzi kama vile mwalimu Dhahabu anamwambia Umu arudi darasani anapoona amekumbwa na mawazo

e)      Mamake kairu ni maskini kwamba kulipa karo ni jambo linalomtatiza ila anaongea na mwalimu mkuu kumruhusu mtoto wake asome akilipa kidogo kidogo

f)        Mwalimu Dhahabu anajishughulisha kuwatafutia mayatima wazazi wa kuwapanga

g)       Shirika la Hakikisho la Haki na Utulivu linajishughulisha katika kusaidia watoto kupata elimu kama ville chandachema

h)      Kituo cha wakfu cha mama Paulina kinamsaidia Zohali aliyepelekwa alipokaribia kujifungua

UKOLONI MAMBO LEO

Ukoloni mamboleo ni zao la uongozi mbaya. Viongozi waanzilishi wa mataifa yaliyopata uhuru hawakuzua sera na mikakati mwafaka ya kuhakikisha nchi zao zimepata kujisimamia kiuchumi. Katika Chozi la Heri, Waafrika wenyewe wanajifanya wakoloni juu ya waafrika wenzao, ambao wako chini yao kitabaka au kisiasa kwa mfano

a)       katika ukurasa wa 5, mashamba ya Waafrika yananyakuliwa na watu binafsi baada ya wakoloni kwenda, nao waafrika wanawekwa mahali pamoja ili kuishi katika hali ya ujamaa “Lakini baba, wewe siwe uliyeniambia kuwa mashamba ya Theluji nyeusi yalikuwa milki ya wakoloni? na sasa yanamilikiwa na nani? Si mwana wa yule mlowezi maarufu ambaye wewe hunitajia kila mara? Maekari kwa maekari ya mashamba katika eneo la kisiwa bora yanamilikiwa na nani? Si yule myunani aliyewageuza wenyeji kuwa maskwota katika vitovu vya usuli wao?”

b)      Katika ukurasa wa 24 tunapata kuwa vijana wanakufa kwa mitutu ya bunduki wanapojaribu kujikomboa kutokana na ukoloni wa Mwafrika. Walipigania uhuru wa tatu, ambao ni ukombozi kutokana na uongozi wa Mwafrika “Baada ya muda mfupi, vifua vyao vilikabiliana na risasi zilizorashiwa vifua hivyo kama marashi, vifua vikawa havina uwezo dhidi ya Shaba, vijana wakaanguka mmoja baada ya mwingine, wame kufa kifo cha kishujaa, wamejitolea mhanga kupigania uhuru wa tatu”

c)       Kampuni zinzazoshinda zabuni za kuchimba madini ni za kigeni n auchimbaji wenyewe unafadhiliwa na wawekezaji wa kigeni amabao huchukua fedha zinazotokana na madini hayo n akuendeleza nchi zakigeni

d)      Waafrika hawawezi kujitatulia matatizo yanayowakumba, inabidi mataifa ya kigeni almaarufu jamii ya kimataifa kuingilia kati n akurejesha Amani baada ya ghasia za baada ya uchaguzi kuzuka nchini wahafidhina

 

ATHARI YA VITA KATIKA NCHI YA WAFIDHINA 

a)       watu kuuawa, kuacha makwao na kukimbilia maisha yao huku kupoteza mali kwani waliokimbia makwao kila walichokiacha kiliteketezwa

b)      kupora maduka ya Kihindi, kiarabu na hata Waafrika wenzao

c)       Misafara ya wakimbizi ikawa kwenye barabara na vichochoro vya Wahafidhina

d)      Mizoga ya watu na wanyama

e)      magofu ya majumba yaliyoteketezwa kwa moto

f)        uharibifu wa mali na mazingira.

g)       Nyimbo za uchochezi mpinzani wa Mwekevu anambiwa tawala wahafidhina, mwanzi wetu tawala.

h)      Kuchomwa kwa magari kana kwamba ni mabiwi ya taka

i)        Vilio kwa waliokuwa wakiteketezwa

j)        Kubakwa kwa mabinti wa Kaizari yaani Lemi na Mwanaheri

k)      Askari wa fanya fujo uone kuwafyatulia risasi vijana walioamua kufa kishujaa.

l)        Magonjwa ya homa ya matumbo

m)    Njaa na ukosefu wa maji safi

n)      Kukimbilia chakula kwa watu wazima jinsi wafanyavyo watoto

UMUHIMU WA MASHIRIKA YA MISAADA

a)       Mashirika ya kidini yanaungana pamoja kuwasaidia waathiriwa kwa kuwapa chakula katika kambi mbalimbali

b)      Kituo cha Benefactor kimeokoa maisha ya watoto wengi k.m Mwaliko, Mtoto aliyeokolewa na Neema na watoto wengine

c)       Shirika la jeshi la wajane la Wakristu linasaidia maisha ya mayatima kama vile Chandachema, Umu na Mwanaheri uk95

d)      Shuleni tangamano iliwasaidia wanafunzi kama vile mwalimu Dhahabu anamwambia Umu arudi darasani anapoona amekumbwa na mawazo

e)      Mamake kairu ni maskini kwamba kulipa karo ni jambo linalomtatiza ila anaongea na mwalimu mkuu kumruhusu mtoto wake asome akilipa kidogo kidogo

f)        Mwalimu Dhahabu anajishughulisha kuwatafutia mayatima wazazi wa kuwapanga

g)       Shirika la Hakikisho la Haki na Utulivu linajishughulisha katika kusaidia watoto kupata elimu kama ville chandachema

h)      Kituo cha wakfu cha mama Paulina kinamsaidia Zohali aliyepelekwa alipokaribia kujifungua

UKOLONI MAMBO LEO

Ukoloni mamboleo ni zao la uongozi mbaya. Viongozi waanzilishi wa mataifa yaliyopata uhuru hawakuzua sera na mikakati mwafaka ya kuhakikisha nchi zao zimepata kujisimamia kiuchumi. Katika Chozi la Heri, Waafrika wenyewe wanajifanya wakoloni juu ya waafrika wenzao, ambao wako chini yao kitabaka au kisiasa kwa mfano

a)       katika ukurasa wa 5, mashamba ya Waafrika yananyakuliwa na watu binafsi baada ya wakoloni kwenda, nao waafrika wanawekwa mahali pamoja ili kuishi katika hali ya ujamaa “Lakini baba, wewe siwe uliyeniambia kuwa mashamba ya Theluji nyeusi yalikuwa milki ya wakoloni? na sasa yanamilikiwa na nani? Si mwana wa yule mlowezi maarufu ambaye wewe hunitajia kila mara? Maekari kwa maekari ya mashamba katika eneo la kisiwa bora yanamilikiwa na nani? Si yule myunani aliyewageuza wenyeji kuwa maskwota katika vitovu vya usuli wao?”

b)      Katika ukurasa wa 24 tunapata kuwa vijana wanakufa kwa mitutu ya bunduki wanapojaribu kujikomboa kutokana na ukoloni wa Mwafrika. Walipigania uhuru wa tatu, ambao ni ukombozi kutokana na uongozi wa Mwafrika “Baada ya muda mfupi, vifua vyao vilikabiliana na risasi zilizorashiwa vifua hivyo kama marashi, vifua vikawa havina uwezo dhidi ya Shaba, vijana wakaanguka mmoja baada ya mwingine, wame kufa kifo cha kishujaa, wamejitolea mhanga kupigania uhuru wa tatu”

c)       Kampuni zinzazoshinda zabuni za kuchimba madini ni za kigeni n auchimbaji wenyewe unafadhiliwa na wawekezaji wa kigeni amabao huchukua fedha zinazotokana na madini hayo n akuendeleza nchi zakigeni

d)      Waafrika hawawezi kujitatulia matatizo yanayowakumba, inabidi mataifa ya kigeni almaarufu jamii ya kimataifa kuingilia kati n akurejesha Amani baada ya ghasia za baada ya uchaguzi kuzuka nchini wahafidhina

 

UKOLONI MKONGWE

Huu ni ukoloni uliokuwa wa Waingereza, kabla ya Afrika kupata uhuru.

a)       Tunapata kuwa mkoloni anapata fursa ya kuendeleza kilimo katika sehemu za mashamba ya Waafrika zilizotoa mazao mengi. Uk 7, “Mustakabali wa ukuaji wetu kiuchumi uligonga mwamba wakati sheria ya mkoloni ilipompa mzungu kibali cha kumiliki mashamba katika sehemu zilizotoa mazao mengi. Ukengeushi wa ardhi ukatiliwa muhuri, umilikajia wa ardhi na Mwafrika katika sehemu hizi ukapigwa marufuku; si mashamba ya chai, si ya kahawa yote yakapata wenyeji wageni dau la mwafrika likagonga jabali.

b)      Katika ukurasa wa 7 tunasoma; “Waafrika waliobahatika kuwa na makao yao binafsi walipata sehemu ambazo hazingeweza kutoa mazao yenyewe; na bila shaka hali yao iliweza kutabirika; kuvyazwa kwa tabaka la wakulima wadogowadogo, maskini, wasio na ardhi. Nadhani unaweza kukisia hali ilivyokuwa kwa familia nyingi za kiafrika. Kama vile baba Msumbili alivyokuwa akisema, jamii yetu iligeuka kuwa hazina kuu ya wafanyakazi ambamo wazungu wangeamua kuchukua vibarua kupalilia mazao yao” Tunaona kuwa wazungu bado waliwatumia waafrika kama wafanyakazi mashambani ‘mwao’, ambayo walinyakua kutoka kwa waafrika.

Kwa kifupi

                                i.            Mkoloni anapuuza sera za mwafrika za umiliki wa ardhi na kuamua kujumuisha pamoja ardhi iliyomilikiwa na mtu binafsi na kuidhinisha umiliki wa hatimiliki

                              ii.            Sheria ya amkoloni inampa mzungu kibali cha kumiliki mashamba katika sehemu zilizotoa mazao mengi

                            iii.            Wazungu wanapiga marufuku umilikaji wa ardhi na waafrika katika sehemu zilizotoa mazao mengi

                             iv.            Waafrika wanalazimika kuwa vibarua katika mashamba yaliyokuwa yao au maskwota amabao maisha yao yalitegemea utashi wa mzungu

                               v.            Wazungu wanachukua waafrika kuwa vibarua vya kupalilia mazao yao wakiwemo watotot wadogo

UTAMAUISHI

Hii ni hali ya wahusika kukata tamaa katika maisha yao au katika jambo fulani. Wahusika mbalimbali waliweza kukata tamaa kwa njia moja au nyingine;

a)       Pete anakata tamaa maishani baada ya kupata watotto watatu akiwa chini ya miaka shirini na moja jambo linalomfanya kutaka kujiua

b)      Wakulima wanakata tamaa baada ya kutopata waliyotarajia baada ya kupata mazao yao. Uk 6; “Sijui ni kwanini hatujaweza kujisagia kahawa au chai yetu itakuwaje mbegu ziwe zetu, tuchanike kukuza zao lenyewe, kasha tumpelekee mwingine kwenye viwanda vyake, aisage tuuzia hiyo hiyo kahawa na chai kwa bei ya kukatiha

c)       Mkewe Ridhaa na familia yake ilipoangamia kwa moto alikata tamaa ya mapenzi katika maisha yake

d)      Zohali licha ya kuzaliwa katika familia ya tabaka la juu anakata tamaa katika maisha na kuingia mtaani kutumia gundi na wenzake

e)      Mwangemi na Neema wanakata tamaaya kupata mtoto na kuamua kupanga Mwaliko

f)        Shamsi anakata tamaa ya kupata kazi na kudhamini pombe licha ya kuwa wa kwanza kuingia chuo kikuu kutoka eneo lao’

g)       Naomi anakata tamaa kuishi na Lunga na kuamua kwenda kutafuta kazi mjini

h)      Naomi anakata tamaa kuishi mjini na kurudi msitu wa samba ila anakuta Lunga aliaga na watoto wakaondoka

i)        Umu anakata tamaa ya kupata nduguye hasa baada ya kugundua kuwa hapati usaidizi katika kituo cha polisi

j)        Mwanaheri anakata tamaa baada ya kifo cha mamake Subira

k)      Subira anakata tamaa ya kuishi kwa Kaizari kutokana na chuki ya mamamkwe kwa kiini kuwa hawakuwa wametoka katika jamii moja

l)        Lunga anakata tamaa ya maisha baada ya kuachishwa kazi, kunyakuliwa kwa mazao yake na kuachwa na mkewe jambo linalosababisha kufa kwake

m)    Chandachema anakata tamaa baada ya nyanya yake kufariki na kunyanyaswa na jirani yake satua

 

 

ELIMU

Haya ni mafunzo yanayotolewa na jamii kwa watu wake. Elimu yaweza kuwa rasmi na kutolewa darasani, au iwe sio rasmi ambayo hutolewa kwenye mazingira ya kawaida yasiyo kuwa ya shuleni au darasani.

a)       Katika ukurasa wa 10; Ridhaa aliungana na vijana wengine kwenda shuleni kupata elimu “Ridhaa alikuwa mmoja wa waathiriwa wa hali hii. Anakumbuka jinsi siku ya kwanza shuleni alivyotengwa na wenzake katika mchezo wao wa kuvuta, mchezo wa kusukuma vifuniko vya chupa ya soda kwa ncha za vidole vyao “Uk 11; “

b)      Ridhaa alipea kwenye anga za elimu, akabisha kwenye milango ya vyuo, akafika kilele cha ufanisi alipohtimu kama daktari “

c)       Mwaliko pia anaendeleza masomo yake hadi akafikia kiwango cha Chuo kikuu. Uk 149; ” Hata alipohitimu masomo yake ya kidato cha nne na kujiunga na Chuo kikuu kusomea shahada ya isimu na lugha, Mwangemi na Neema walijua kuwa juhudi zao za malezi hazikuambulia patupu “

d)      Mwangeka anapatikana akienda shuleni kupata Elimu. Tunaambiwa kuwa Jumamosi moja, Mwangeka alikuwa ametoka shuleni, na siku hizo walimu walikuwa wameng’ang’ania kuwafunza Jumamosi wanafunzi waliokaribia ‘ICU’,kama walivyoliita darasa ala nane (uk 59).Mwangeka anaonekana kuendeleza masomo yake hadi Chuo kikuu na baadae kuajiriwa kazi (uk 62.)

e)      Lunga Kiriri Kangata naye anapata elimu yake, kwani tunapata kumuona kama amri-jeshi wa uhifadhi wa mazingira walipokuwa shuleni. Tunaambiwa kuwa kila Ijumaa wakati wa gwaride, Lunga angehutubia wanafunzi wenzake na walimu kuhusu swala la mazingira (uk 67-68).

f)        Umulkheri pia anaenda kupata elimu yake katika shule. Tunampata mwalimu wake akijaribu kumrejesha Umu darasani wakati fikra zake zinapo ondoka katika shughuli za masomo. Tunapata pia kuwa kwa hali ambayo Umu alikuwa akiishi, mwalimu mkuu wa Shule ya Tangamano, anamsajili kuwa mwanafunzi huko, kwa hisani yake na kwa ushauri wa wizara ya elimu (uk 78). Umulkheri anayaendeleza masomo yake hadi Chuo kikuu, anapoenda ughaibuni kusomea huko (uk 128).

g)       Mhusika Pete pia anatumika katika kuwasilisha maudhui ya elimu, ingawa elimu yake inagonga mwamba baada ya kuozwa kwa mzee mmoja aliyeitwa kuwa katika darasa la saba, wazazi wake walipomuoza kwa mzee huyu.

h)      Baada ya Naomi kuhangaika kwa miaka mingi akiwatafuta watoto wake, anaamua kuanzisha biashara ndogo karibu na Chuo kikuu cha Mbalamwezi, na kazi anayoifanya ni kuwapigia wasomi chapa na kuisarifu miswada yao. Kwa hivyo, tunapata kuwa maudhui haya ya elimu yanajitokeza pia, kwa kuwepo kwa Chuo kikuu (uk 193).

i)        Masomo ya Mwangeka ya chuo kikuu yanamkutanisha n amkewe lily nyamvula aliyekuwa akisomea shahada ya uanasheria

j)        Elimu humsaidia mtu kuchagua taaluma, watu wanaamini kuwanuanajeshi ulitengewa tu watu wa viwango vya chini vya elimu

k)      Babake shamsi anahangaika kufanya kibarua kwenye shamba lililokuwa lake lilonyakuliwa na bwana mabavu ili kumlipia shamsi karo

l)        Shamsi ndiye wa kwanza kijijini kufuzu kuotoka chuo kikuu licha ya kukosa kazi

m)    Pete anakosa kwenda shuleni kwa juma moja kwa sababu ya kukosa sodo

 

UONGOZI

Haya ni madaraka anayopewa mtu ya kusimamia au kuongoza shughuli fulani. Anayepewa mamlaka haya anakuwa ndiye kiongozi. Uongozi waweza kuwa mbaya au uongozi mzuri.

a)       Tunapata kuwa watu wanachagua viongozi wanaotaka, na kampeni pia zinafanywa kwa njia ya kutupa vikaratasi ovyo ovyo. Uk 12;”Sasa ameanza kuelewa kwa nini wiki iliyopita vikaratasi vilienezwa kila mahali vikiwatahadharisha kuwa mna gharika baada ya kutawazwa kwa Msumbi ( kiongozi) mpya. “Siku ile baada ya kutawazwa kwa kiongozi mpya, kiongozi ambaye kulingana na desturi za humu mwetu, hakustahili kuiongoza jamii ya Wahafidhina, kisa na maana alikuwa mwanamke, mbingu zilishuka “

MAPENZI.

Hii ni hali ya mvuto na upendo alionao mtu kwa mtu mwingine. Pia nia hisia ya upendo anayokuwa nayo mtu kuhusu mtu mwingine.

b)      Ridhaa alimpenda sana mkewe Terry na wana wake. “Polepole parafujo za mwili wake zililegea, akaketi juu ya ma. jivu-la, juu ya miili ya wapenzi wake “

c)       Tunapata kuwa kuna mapenzi kati ya Mwangeka na baba yake Ridhaa. Haya ni mapenzi ya mzazi kwa mwanawe, Ridhaa alimpenda sana mwanawe Mwangeka kwani ndiye pekee tu aliweza kuepukana na janga Ia mauti kwa familia yote yake Ridhaa. Mapenzi haya yanadhihirika wakati Ridhaa anamlaki mwanawe kwenye uwanja wa ndege anapokuwa akirudi nyumbani kutoka ughaibuni. Wanaonekana wakikumbatiana kwa muda na Mwangeka kujitupa kifuani mwa babake, – na wanashikana kukutu. Pia wanazungumza kimoyoyo kuhusu jinsi maisha yao yamekuwa; kwa kweli haya ni mazungumzo ya wapendanao (uk 46- 47).

d)      Maudhui ya mapenzi pia yanajitokeza kati ya Billy na sally. Sally alikuwa msichana ambaye Billy alichumbia kwao, na kisha akamleta katika nchi hii ya kiafrika ili kumuonyesha mahali wangeweza kuishi baada ya kufunga akida. Kwa bahati mbaya, Billy anasalitiwa na mpenzi wake sally na kuambiwa kuwa jumba lenyewe ni kama kiota cha ndege, mahali ambapo yeye hawezi akaishi hata kuwe vipi (uk 80).

e)      Tunapata pia kuna mapenzi kati ya Subira na wanawe Mwanaheri na Lime. Hili linajidhihirisha baada ya Subira kumwandikia barua mpenzi mwanawe Mwanaheri. Haya ni mapenzi ya uzazi lakini Subira anawasaliti wanawe (uk 95.)

f)        Pia kuna mapenzi kati ya Umulkheri na wazazi wapya wa kupanga, Mwangeka na mkewe Apondi anaowapata baadae. Mwangeka na Apondi wanampenda sana Umu ni kusema kuwa ni baraka za Mungu za kumfidia mwana wao aliyeaga dunia. Umulkheri naye anawapenda sana hawa wazazi wake wapya kwani waliweza kumlipia hafi karo. Pia waliweza kumponya uchungu aliokuwa nao moyoni wa kuachwa na wazazi wake (uk 117-118)

g)       Kuna mapenzi yanayojidhihirisha katika familia hii ya Mwangeka na Apondi, kwa wana wao. Wakati umulkheri anafikiwa na wakati wa kwenda kuyaendeleza masomo yake ughaibuni, wanamsidikisha hadi kwenye uwanja wa ndege. Mapenzi makali yanajidhihirisha wakati kila mmoja wao analia machozi kwa kuachana na Umu alipokuwa akiliabiri ndege Tumaini (uk 128).

h)      Kuna mapenzi kati ya Mwaliko na wazazi wake wa kupanga ambao ni Bwana Mwangemi na Bii Neema, ambao hawakuwa na uwezo wa kukilea kizazi chao, na hatimaye wakaamua kumpanga mwana huyu ili awe wao rasmi. Hawa wawili wanampenda sana Mwaliko, naye Mwaliko anawapenda kama wazazi wake halisi (uk 166-167).

i)        Naomi anawapenda sana watoto wake ingawa alikuwa amewasaliti kwa kuwaacha wakiwa wachanga. Ameishi kuwatafuta walikopotelea kwa miaka mingi, lakini mwishowe, anawapata wana wake bado wako hai na wamejiendeleza sana kimaisha na kimasomo. Anawaomba msamaha huku akiwa na uchungu mwingi rohoni mwake. Wana wake wanamsamehe mwishowe kwa mapenzi waliyokuwa mamayao (uk 192-193)

j)        Mwangeka anampenda sana mke wake mpya apondi uk 109

k)      Neema anamwonyesha mwaliko mapenzi kwa kumkumbatia huku akitokwa na machozi ya furaha uk 167

l)        Katika hadithi ya tindi na lemi, mama yao anakumbwa na mawazo kuhusu mahali waliko wanawe. Anachukua hatua kupiga ripoti kwa vituo vyote vya polisi kisha baadaye anasalia kumuomba mungu awalinde wanawe uk 167