1. a) 'Mimi ni mwanamume. Ninaweza kuoa wakati wowote na idadi yoyote ya wanawake. Shida iko wapi'? Mwanamke akishaolewa, basi. Yake yamekwisha hapo. Azae na kuitumikia jamaa yake bila kuulizauliza maswali.'
i. Weka dondoo hili katika muktadha wake.
ü Ni maneno ya Mrima.
ü Anamjibu Mangwasha mkewe.
ü Wako nyumbani kwao.
ü Mangwasha almuulza ikiwa Sagilu anamtafutia mkc mwingine kisiri
ii. Fafanua sifa sita za msemaji wa maneno haya. (alama 6)
Mrima
ü Mtamaduni- anasema mila hairubusu ycye akatunzwe na mkc
kama ngonjwa.
ü Mbadhirifu- anafuja pesa na mwanamkc njc ya ndoa.
ü Mzinzi- ana mwanamke nje ya ndoa-
kutoka kwa barua.
ü Hajawajibika- anatowcka nyumbani na kumwachia Mangwasha majukumu ya nyumbani.
ü Nadhifu-
alivaa na kubadilisha suti kila uchao.
ü Mcheshi- akikosckana kazini watu waliteta.
ü Karimu- alihudumia watu bila uchoyo.
ü Mwenyc bidii- biashara ya uchuuzi na duka
ü Mbaraza- mtu wa watu
ü Mlevi- anakesha vilabuni vya pombe.
b). Maudhui ya usaliti yamejadiliwa kwa kina katika Riwaya nzima. Thibitisha
üMtemi Lesulia amesaliti jamii ya Waketwa kwa kuibagua katika ajira inayowaendea
Wakule pekee.
ü Mtemi Lesulia amesaliti nchi kwa kuzorotesha uchumi kupitia ufisadi na sera mbovu
ü Mtemi Lesulia amesaliti uaminifu wa Ngoswe kwa kuwaambia vijana wenzake wavuruge
amani wakati wa uchaguzi ili ushindi umwendee
Sagilu bila kujali usalama.
ü Mtemi Lesulia amesaliti hakimu kwa kumnyang'anya cheti na kumfuta kazi licha ya
kufanya kazi kulingana na sheria.
ü Mtemi Lesulia amesaliti imani ya marafiki zake kwa kuwafukuza walipofika kwake kumpa pole kwa kushindwa kwenye uchaguzi.
ü Sagilu amesaliti jamii ya Waketwa walioishi Matango kwa kushiriki kuchoma makazi yao licha ya kuwa alitaka achaguliwe kama mbunge.
ü Sagilu amesaliti Mrima kwa kumhonga pesa ili ashiriki ulevi akijua kuwa alimtaka mkewe
Mrima mapcnzi.
ü Sagilu amesaliti Mangwasha kwa kumtembelea akijifanya anajali lakini ndiye alifadhili mumewe Mrima ashiriki ulevi hadi
akafutwa kazi.
ü Sagilu amesaliti anamsaliti mwanaye Mashauri kwa kumnyang'anya mchumba Cheiya.
ü Sagilu amesaliti Mtemi Lesulia kwa kumhakikishia kuwa kila kitu kiko shwari katika uchaguzi huku akijua kuwa hangeshinda.
ü Sagilu amesaliti Mtemi Lesulia kwa kuzaa na mkewe Nanzia huku akijifanya rafiki yake
ü Sagilu amesaliti jamii ya Matuo kwa kuwauzia watoto maziwa yenye
sumu bila kujali yangewadhuru vipi.
ü Cheiya anamsaliti mchuimba wake Mashauri kwa kujihusisha kimapenzi na Sagilu babaye
Mashauri.
ü Nanzia anasaliti
jamii ya
Matuo
kwa
kuhodhi mali
ya umma kwa manufaa yake
binafsi/kuchoma makazi yao ili
afaidi ardhi.
ü Nanzia anasaliti mumewe Mtemi Lesulia kwa kufanya mapenzi na Mhindi na Sagilu
ü Sagilu amesaliti Mtemi Lesulia kwa kuzaa na mkewe Nanzia huku akijifanya rafiki yake
ü Cheiya anamsaliti mchuimba wake Mashauri kwa kujihusisha kimapenzi na Sagilu babaye
Mashauri.
ü Nanzia anasaliti
jamii
ya Matuo kwa kuhodhi
mali ya
umma
kwa
manufaa
yake binafsi/kuchoma makazi yao ili afaidi ardhi.
ü Mbwashu anasaliti
Mtemi Lesulia kwa kumtoroka na
kwenda Ulaya
anaposhindwa nawalifanya maovu mengi pamoja.
ü Chifu Mshabaha anasaliti Waketwa kwa kushiriki njama ya kuwaondoa makao yao.
ü Chifu Mshabaha anamsaliti Mangwasha kwa kuleta msichana mwingine kazini ili kumfuta
yeye kazi.
ü Mrima anasaliti mkewe Mangwasha kwa kushiriki mapenzi nje ya ndoa/anashirikiana na Sagilu huku mkewe akiteseka.
ü Mrima anasaliti Mangwasha na akina Lonare anapochukua hongo ili amfanyie Mtemi
Lesulia kampeni ilhali
anajua huyu ni adui ya Waketwa.
2. Matatizo ya Afrika ni tokeo la uongozi mbaya. Thibitisha kwa kurejclea riwaya ya Nguu za Jadi. (alama 20)
ü Uhaba wa ajira- vijana waliokamilisha masomo wanakosa ajira na
wengine
wanaonekana na Mangwasha wakiwa katika maeneo ya maduka
wakipitisha wakati.
ü Kufutwa kazi kiholela- Mangwasha anafutwa kazi bure katika ofisi ya chifu Mshabaha wa kuunga mkono lonare.
ü Ukiritimba wa kiuchumi- wenye ushawishi kama akina Sagilu wanamiliki nyenzo zote
ü muhimu za kiuchumi k.v
mashamba, vituo vya petrol
na msururu wa maduka ya
jumla.
ü Unyakuzi wa
ardhi- Sagilu na Lesulia
wanapanga njama
ya kunyakua ardhi ya Wanamatongo badala ya kuwatetea.
ü Unyakuzi wa mali ya umma- Nanzia mkewe Mtemi Lesulia ananyakua jengo moja refu
katikati
ya mji na kubadilisha jina kuwa Skyline Mall.
ü Ubaguzi-
Utawala wa
Lesulia kuajiri tu
Wakule hata
wale
hawajahitimu
vilivyo na kubagua Waketwa.
ü Ukabila- Mshabaha kuajiri watu wengi wa kabila lake
ü Kunyanyasa wapinzani- magari ya Lonare yanashikwa bila hatia ila ni kwa sababu anampinga Mtemi
Lesulia.
ü Uharibifu wa mazingira- matajiri wanachimba mawe na wengine kumiliki karakana za
machimbo ya
mawe.
ü Ufisadi/ hongo- chifu Mshabaha anapokea hongo ili aridhiane na serikali ya Mtemi Lesulia kuinyakua ardhi ya Matango kufuatia misingi ya kisiasa.
ü Kuchoma
nyumba- nyumba za
Waketvwa kama vile Mangwasha zinachomwa
kwa misingi ya kikabila na kisiasa.
ü Mishahara duni- Mangwasha anapata mshahara usiokimu familia yake.
ü Bidhaa ghushi- Sagilu anaagiza maziwa yaliyotiwa sum una kuhatarisha maisha ya
watoto wengi.
ü Biashara haramu- madanguro
ü Ukosefu wa haki kuamua kesi- Mafamba ni wakili laghai wa serikali- inashinda kesi mbalimbali
ü Utekaji nyara- utawala wa Lesulia unamteka nyara Lonare ili asishindane naye katika uchaguzi.
ü Kutumia vijana kuzua vita- Lesulia kuwapa vijana fedha ili wahonge watu siku ya
uchaguzi na kuzua fujo katika vituo vya Majengo na Matango ambavyo vilikuwa na ufuasi
mkubwa wa Lonare.
ü Siasa za chuki- Lesulia hakutaka upinzani
ndio maana ana chuku kwa Lonare mpinzani wake.
ü Mfumuko wa bei- bei ya bidhaa muhimu imepanda katika nchi ya Matuo na kuwafanya
ü watu wa tabaka la chini kama Mangwasha kushindwa kuzimudu.
ü Ulanguzi wa mihadarati- Ngoswe, mwanawe Mtemi
na watu wengine wenye ushawishi wanamiliki mtandao mkubwa wa ulanguzi wa dawa za kulevya na
kudhuru afva za
wananchi
ü Ulanguzi
wa
mihadarati-
Ngoswe, mwanawe Mtemi na watu wengine wenye ushawishi
3. “Samahani… Nina shida kidogo. Ninaomba usaidizi. Sikuwa nikilipa ushuru katika biashara zangu. Sasa wanataka kuzifunga na kunipeleka kotini.”
a) Eleza muktadha wa dondoo
ü Haya ni
maneno ya Chifu Mshabaha
ü Akimwambia Mangwasha
ü Ofisini
mwa
Mangwasha mjini
ü Alikuwa ameenda kumwoba msaada kama angemsaidia kumtetea katika ofisi za kiserikali ahurumiwe kutolipa ushuru
na biashara zake zisifungwe.
b) Bainisha toni katika dondoo hili (alama 2)
ü Toni ya kurai-samahani
ü Toni ya masikitiko-sasa wanataka kuzifunga na kunipeleka kortini.
ü Toni ya uoga –naomba
usaidizi.
c) Msemaji wa maneno haya na wengine ni adui ya wananchi wa Matuo. Eleza ukweli wa kauli hili. (alama 14)
Chifu Mshabaha
ü Ufisadi - Chifu Mshabaha na wengine wanapanga kuitwaa ardhi ya mtaa wa Matango kwa
manufaa yao wenyewe.
ü Kuwateka nyara wapinzani wa Lesulia-Lonare anatekwa nyara na kupigwa sana siku chache kabla ya uchaguzi na Serikali ya Lesulia.
ü Uzinzi-Sagilu anashiriki uozo huu na Cheiya.
ü Kuwadhulumu wanawake - Sagilu anamtaka mapenzi Mangwasha akijua tayari amechumbiwa na Mrima na anapomkataa Sagilu anafanya
kila
juhudi kuismbaratisha
ndoa
ya hawa wawili.
ü Kupanga kuwafurusha Waketwa kutoka Matango kwa sababu ya tamaa ya mali na uongozi.
ü Kuwaua watu- Sihaba anatumwa na Sagilu kumwangamiza mwanabiashara mkubwa wa
sariji kwa kijana Kifaru-huu ni ukatili.
ü Kuuza bidhaa
haramu na hatari kwa wananchi - Sagilu anaagiza maziwa
ya
watoto yaliojaa vijasumu ili yasiharibika haraka.Watoto wanapoyatumia wanaathirika sana.
ü Kupitia kwa Mahauri mtaalamu mkuu wa usanifu wa majengo jijini Taria anaidhinisha ubomoaji wa jingo la Lonare.
ü Viongozi walichochoea ukabila katika ofisi za umma-
Chifu Mshabaha anamfuta kazi
Mangwasha kama mhazili wake wa miaka nyingi
na kumwandika kazi msichana wa
kabila lake.
4. Hivyo, alitaka kubadili hali hata kama ilimaanisha kukitia kichwa chake kinywani mwa samba. Alitaka kuliokoa jahazi lililokuwa likielekea mwambani kwa kasi. Lakini angeliweza vipi kupambana na utandu wa mahasisi hao?
a) Eleza mbinu nne za mimtindozinazojitokeza katika dondoo
ü Taswira-lililokuwa likielekea mwambani
ü Jazanda-kukitia kichwa chake kinywani mwa samba
ü Swali balagha.-lakini
angeliweza vipi kupambana na utandu wa mahasidi hao?
ü Nahau- kuliokoa jahazi
b) Eleza sababu za mrejelewa kutaka kufaulisha kauli iloyopigiwa mstari (al 10)
ü Ufisadi umekithiri katika nchi ya Matuo. Watu wenye ushawishi
kama Sagilu hawakulipa
kodi na waliagiza
hata bidhaa hatari kama maziwa ya watoto yenye sumu.
ü Kulikuwa na ukabila - Mangwasha anaeleza jinsi waajiiwa wengi katika ofisi ya chifu walikuwa wa kabila lake mshabaha.
ü Ubaguzi katika
ajira - Utawala wa mtemi unawabagua waketwa wakati wa ajira.
ü Uhaba wa ajira - Vijana wengi waliokuwa wamehafilika kutoka taasisi
za elimu walikosa
kazi.
ü Ukiritimba wa kiuchumi - Sagilu anamiliki nyenzo
zote muhimu za kiuchumi
ü Unyakuzi
wa
mali ya umma - Nanzia ananyakua jengo moja refu katikati ya mji.
ü Unyakuzi
wa
ardhi ya wanajamii - Sagilu napanga kunyakua ardhi ya
wanamatango.
ü Kufutwa kazi kiholela - Mangwasha anapigwa kalamu katika ofisi ya chifu kwa kuunga
mkono kampeni za Lonare.
ü Mshahara mdogo kwa wafanyikazi - Mshahara anaolipwa Mangwasha haukuhudumia familia yake.
ü Ukosefu wa elimu miongoni mwa vijana -
Mangwasha aliwaona vijana wakizurura
mtaani.
ü Kutelekeza watoto wa kiume na kuishia kuingilia matumizi ya dawa za kulevya.
ü Watoto
wa kike wanatumiwa katika biashara
ya
ngono.
Sihaba anamiliki danguro anapotumia wasichana wadogo.
ü Ulanguzi wa mihadarati
- Ngoswe namiliki
mtandao wa ulanguzi wa dawa za kulevya.
ü Matumizi ya pombe haramu - Mrima wanabugia pombe harmu
ü Ukware. Sagilu anajihusisha kimapenzi na Cheiya ingawa ana mke.
ü Utekaji nyara. Utawala wa Lesulia unamteka nyara Lonare ili asishindane naye katika
uchaguzi.
ü Uharibifu wa mazingira. - Viongozi walichimba mchanga na kukata miti bila kujali.
c) Eleza umuhimu wa mrejelelewa katika kujenga ploti ya riwaya hii (al 6)
Ngoswe
ü Mlanguzi wa dawa za kulevya – anauza dawa za kulevya hata Lonare anamwambia
aache
ü Mpyaro – anamtusi Sagilu Mzinifu
– anamweleza rafikiye Mashauri kuwa hafai kuwa na mpenzi
mmoja kama alivyo na Cheiya tu.
ü Mbadhirifu – anasemekana kutumia pesa za kodi anayokusanya kutoka kwa nyumba za babake ovyo
ü Mpenda anasa
– anasemekana kuwa na vilabu
vya ulevi. Pia anajihusisha na wasichana
wengi vilabuni
(b) Jadili umuhimu wa msemewa wa kauli hii
Mashauri
ü Anajenga ploti. Anakosana na Cheiya kwa sababu ya usaliti wake.
ü Anaendeleza maudhui mbalimbali. Anaendeleza maudhui ya mabadiliko kwa jinsi
anavyohusiana na babake. Pia anaacha kushirikiana na serikali na kujihusisha na upande
wa
Lonare.
ü Anajenga sifa za wahusika wengine. Anajenga sifa za Cheiya kama saliti. Cheiya ambaye
ni mpenziwe anamsaliti kwa kujihusisha na babaye.
ü Anakuza migogoro mbalimbali katika riwaya. Anakuza mgogoro wa kimapenzi, kisiasa n.k.
ü Anaonyesha namna usaliti unavyoweza kuleta uhasama kati ya watu wa jamii/familia
moja. Anakosana na babake kwa kumsaliti na mpenziwe.
ü Ni kielelezo cha watu ambao wanabadilika kimsimamo wanapotambua makosa yao.
ü Baada ya kutambua uovu wa serikali ya Lesulia, anajitenga nao na kujiunga na Lonare.
(c) Wanaosemekana kushikana mikono wanaendeleza uozo katika jamii. Thibitisha.
Sagilu na Cheiya
ü Sagilu anaendeleza ufisadi kwani anauzia watu bidhaa ghushi. Alileta maziwa ya watoto ya viwango vya chini na yenye
sumu.
ü Sagilu anawanyanganya
watu wake zao. Wake zake wote walikuwa mabibi za watu.
ü Sagilu alizini na Cheiya ambaye alikuwa mpenzi wa mwanawe
ü Sagilu anapata mtoto na Nanzia ambaye ni mke wa mtemi.
ü Sagilu anataka kuvuruga ndoa ya Mrima na Mangwasha. Alimpa Mrima pesa akasahau majukumu yake.
ü Sagilu anawalipa watu kwenda kumteka nyara Lonare kwa nia ya kumuua.
ü Sagilu anahusishwa na kupanga njama ya kuharibu
kampeni za Lonare.
ü Sagilu anahusishwa na uchomaji nyumba za waketwa.
ü Cheiya anatumwa kumuua Lonare kwa kumwekea sumu katika kinywaji
ü Cheiya anamsaliti mpenziwe kwa kujihusisha kimapenzi
na Sagilu
ü Cheiya anasemekana nujihusisha na Mashauri kwa sababu ya pesa zake na si mapenzi
(d) Bainisha mtindo katika dondoo.
ü Kuchanganya ndimi – I say, wajua nimewaona wapi
leo?
6. Mandhari ya afisi ya Chifu Mshabaha ni muhimu sana katika riwaya hii ya Nguu za Jadi. Onyesha namna mandhari hayo yanajenga;
(a) Maudhui mbalimbali
ü Ufisadi – chifu halipi ushuru
ü Hila/njama –kuna watu walipanga njama/mkutano wa siri
wa
kuchoma nyumba za
waketwa
ü Ubaguzi –chifu anabagua waketwa. Ameajiri
wakule wengi katika afisi yake. Mangwasha pekee ndiye mketwa na anafanya majukumu mengi
ü Ukabila
–chifu anamchukia Mangwasha na Mrima kwa kuona
kuwa wanaoana Unyanyasaji/dhuluma –chifu anamdhulumu Mangwasha kwa kumwachisha kazi ovyo
ü Ubarakala
–chifu anafanya kila kitu kumpendeza Mtemi na Sagilu badala ya kuwalinda
wananchi
ü Uwajibikaji –Mangwasha anasemekana kuwajibikia kazi yake pale afisini. Hakuzembea.
ü Ndoa –Mangwasha na Mrima wanapatana pale afisini na kuwa marafiki hadi kuoana/mangwasha anaomba
ruhusa ya siku chache pale afisini ili
aende kufunga ndoa na Mrima.
ü Ukatili – kuchomea waketwa nyumba
ü Siasa mbovu/uongozi mbaya –afisi ya chifu inaathiri siasa kwani
inapanga kumsaidi Sagilu
na Mtemi ili wawashide wapinzani wao.
ü Unyakuzi –stakabadhi za kuchangia kesi ya kulinyakua shamba la watu wa matango zilipatikana katika afisi hii
ü Unafiki –chifu Mshabaha anajidai kuwa wao ni wasamaria wema wa kumwauni Mangwasha ila sivyo
ü Mapenzi –mapenzi baina ya Mrima na Mangwasha yalianzia hapa
ü Siri –mikutano mingi ya kisiri
ilifanyika hapo na Sagilu
ü Usaliti
–Chifu Mshabaha anawasaliti wananchi wa eneo lake la kazi kwa kujiunga na wachomaji nyumba za waketwa.
(b) Migogoro ya aina mbalimbali.
ü Mgogoro wa kikazi/kazini baina ya Mangwasha na Chifu Mshabaha/serikali
ü Mgogoro wa kikabila baina ya waketwa na wakule
ü Mgogoro wa kimapenzi/ mapenzi
baina ya Mangwasha, Mrima na Sagilu
ü Mgogoro wa
kiutawala baina ya Chifu Mshabaha na serikali kuu kwa kukosa kumhakikishia Sagilu ushindi. Pia baina ya Mangwasha na serikali kwa chifu kumwachisha kazi kwa
kujihusisha na upinzani.
ü Mgogoro wa kikazi/kazini baina ya Mangwasha na Chifu Mshabaha/serikali
ü Mgogoro wa kikabila baina ya waketwa na wakule
ü Mgogoro wa kimapenzi/ mapenzi
baina ya Mangwasha, Mrima na Sagilu
ü Mgogoro wa
kiutawala baina ya Chifu Mshabaha na serikali kuu kwa kukosa kumhakikishia Sagilu ushindi. Pia baina ya Mangwasha na serikali kwa chifu kumwachisha kazi kwa
kujihusisha na upinzani.
ü Mgogoro wa kimapenzi baina ya Mrima/Mangwasha na Sagilu kupitia kwa chifu. Chifu
anamtusi na kumdhihaki Mangwasha kwa kumkataa Sagilu.
ü Mgogoro wa kisiasa baina ya waketwa na wakule. Chifu anajihusisha katika maswala ya
kisiasa ili kuhakikisha Sagilu amechaguliwa.
ü Mgogoro wakiuchumi kwani inasemekana kuwa Chifu ni miongoni mwa watu wasiolipa ushuru
nchini.
7. Yapimeni maneno ya … ‘Hata kama tuna ushahidi huu, tangu lini panya akashinda kesi mbele ya baraza la paka?”
(a) Fafanua muktadha wa maneno haya. (al 4)
ü Msemaji – mangwasha
ü Msemewa – lonare, sagura na mbungulu
ü Mahali – wako kwenye hema la mangwasha/kwa mangwasha
ü Hii ni baada ya mangwasha kuona kuwa kesi hiyo itakuwa ngumu kwa kuwa mwasisi
wake ni mtemi.
(c) Onyesha jinsi akina ‘panya’ walivyonyimwa haki katika riwaya hii.
ü Kufurushwa – wakazi wa matango wanafurushwa kutoka kwao kufuatia sababu
za kisiasa.
ü Kushambuliwa – Lonare amekuwa akipangiwa mauaji na viongozi wakule kama vile Mtemi Lesulia ila ameepuka mitego hiyo ya hatari.
ü Kudhalilisha -
Chifu Mshabaha anamdhalilisha
mangwasha kwa kumtusi. Anamwambia kwenda! Waketwa ni
watu wasio na akili hata ya kuwachagua wachumba.
ü Kufutwa kazi – mangwasha anafutwa kazi na chifu Mshabaha bila kuwepo kwa sababu maalum.
ü Kuchomewa nyumba – waketwa wanachomewa nyumba zao eneo la matango kwa sababu za kisiasa na wanakosa mahali pa kulala na wanasumbuka kwa baridi.
ü Kutekwa nyara – Lonare anatekwa nyara na Mtemi Lesulia ili kuharibu mpango wake wa kupigiwa kura.
ü Kuharibu mali
yao
– mashauri analibomoa jengo la Lonare kwa sababu
za kisiasa.
ü Kunyimwa nafasi za ajira – Serikali ya Mtemi Lesulia inakosa kuwaajiri vijana Waketwa waliohitimu kwa sababu ya ukabila.
ü Unyakuzi wa ardhi yao – Mtemi Lesulia anayakua ardhi ya Matango ili ampe mke wake Nanzia na Mbwashu kibaraka wake.
ü Kuhangaishwa na polisi – Magari ya Lonare yanashikwa bila sababu na hata madereva wake
kushikwa kwa makosa yasiyoeleweka.
8. Ole wako ewe mwanaume uishiye leo. Unaye chakura mapipa ili kuizima njaa uliikosea nini jamii hata usalie kuwa ombaomba? Umevaa koti kuukuu na umesalia kuwa nyuma kama koti hilo. Yu wapi baba aliye kutelekeza? Wapi jamii isiyothamini elimu na utu wako? Jamii ilimshika mkono mtoto wa kike. Ikapiga mbio na mtoto wa kike. Ikasahau kwamba hata wewe unastahili kushikwa mkono. Lazima tujirudi tuone ni wapi tulipoanza kupotea njia. Lazima tuokoe kizazi hiki kinacho potea nyikani bila matumaini. Ole wako matuo, utashika mti gani?
a) Changanua mtindo katika dondoo hili. (alama 10)
ü Taswira – kuchakura mapipa
ü Swali balagha – usalie kuwa ombaomba?
ü Tashhisi – matuo kushika
mti gani.
ü Majazi – matuo
– kusonga mbele ambapo nchi ya matuo haisongi mbele kwani inakumbwa na changamoto nyingi
mf.
Umaskini, ukosefu wa ajira.n.k.
ü Msemo – kushika mkono
ü Tashbihi/tashbiha – kusalia nyuma kama koti
ü Uzungumzi nafsi-ole wako matuo utashia mti gani?
b) Juhudi za kuzuia ufanisi wa jamii ni juhudi za mfa maji. Jadili (al 10)
ü Chifu mshabaha anataka amchagulie Mangwasha mume na amlazimishe aolewe na Sagilu ila Magwasha anakataa na anaolewa na Mrima.
ü Sagilu alimfahamu na kumdharau sana Mrima ila ndiye anayemuoa Mangwasha ambaye anamkataa mume huyu aliye na mali.
ü Mbungulu anakanya Mangwasha
kwenda
Ponda
mali kumtafuta mumewe,
Mrima, aliyepotelea ulevini kwa madai kuwa utamaduni hauruhusu ila Mangwasha anapuzilia mbali utamaduni huo potovu na naelekea huko kumtafuta. (uk.32)
ü Uongozi wa Mtemi Lesulia unawanyima waketwa kazi ila kuna wale wanaobahatika na
kupata ajira katika kampuni za kibinafsi huku wengine wakianzisha biashara zao. (uk.45)
ü Lonare anawakabili wapinzani wake; Sagilu, Mbwashu, Chifu
mshahaba hotelini Saturn na
kumkabidhi bahasha yake yenye pesa za hongo.
ü Lonare Anawaongoza watu wake wa jamii ya waketwa kwa ujasiri licha ya vitisho na mitego ya vifo kutokana na mashambulizi ya watu waliotumwa kumwangamiza.
ü Lonare alishambulia maovu ya kijamii kwa ukakamavu bila kuogopa serikali dhalimu ya Mtemi Lesulia.
ü Akiwa kiongozi wa upinzani; Lonare anahujumiwa katika biashara
na majengo yake, anatekwa nyara na kuteswa ili
asishiriki kwenye uchaguzi
ila
anashiriki na kushinda kura.
ü Wakati wa uchaguzi uliopita Lonare alitekwa nyara na kuteswa na hakutetereka akaendelea kuwa mpinzani katika uchaguzi
wa
sasa.
ü Lonare hajali ukabila uliopo nchini Matuo na hata anamwajiri mbaji kuwa meneja wa kampuni
ya mabasi yake ilhali Mbaji ni Mkule naye ni Mketwa na jamii hizi zilichukiana
ü Magari
yake Lonare ya usafiri yanapokamatwa kwa visingizio visivyokuwa na maana hadi madereva wake kutozwa faini zisizoeleweka, havunjiki moyo bali aliendelea na biashara hiyo.
ü Lonare anawaelimisha wanawe wote bila ubaguzi wa kijinsia katika jamii
hii iliyojaa ubabedume.
ü Licha ya kuwa kuna ukabila na anaukemea ukabila huku akitaka watu wote watendewe haki.
ü Lonare anapigania haki kwa waketwa wanaochomewa makazi yao na kufurushwa Matango
hasa pale anapoungana na Mangwasha kupeleka kesi
mahakamani.
ü Cheiya alitaka kumuua Lonare
wakati mmoja ila akashindwa
na Lonare anapomwona, anataka akamatwe kwa kosa hilo.
ü Cheiya alijaribu kukimbia ila baadaye aliweza kukamatwa na kufikiswa kwenye kituo cha polisi. (uk 156,157)
ü Sagilu anashiriki na Mtemi Lesulia pamoja na Chifu Mshabaha ardhi ya waketwa eneo la
Matango, anaishia kupoteza kura ya ubunge.
ü Sihaba anafanya biashara ya ukahaba kwa kutumia wasichana wadogo, kupitia Mangwasha
na Mrima, watoto hawa wanaokolewa hiyo kufungwa na Sihaba anatiwa mbaroni. (uk
141,142)
ü Sihaba alitaka kuwaangamiza Mrima na Mangwasha katika harusi yao, anagundulika na anakimbilia usalama wake na anafaulu kutoweka.
ü Mangwasha na Mbungulu wanamwona Sagilu akiwa amerukwa kichwa na Mangwasha
anasema kuwa ni kutokana na uovu alioufanyia watu ndipo akawa mwendawazimu; ulikuwa msiba wa kujitakia.
9. ‘Habari hizo nimeshazipata tangu juzi. Mwakala wangu hawalali. Wala hayo yasikutie tumbo joto’
a) Weka dondo hili katika mukthadha wake (alama 4)
ü Haya ni
maneno ya Lonare
ü Anamwambia Mangwasha.
ü Wakiwa ofisini mwa chifu Mshabaha
ü Wanazungumzia kuhusu vijikaratasi vilivyo – sambazwa ili kuhamisha waketwa.
b) Msemaji wa maneno haya anaendeleza vipi maudhui mbalimbali katika riwaya hii? (alama 6)
ü Dini
- Lonareanasema kuwa mlinzi wake ni mungu na wapili ni wafuasi wake.
ü Uzalendo – anawania uongozi ili
atetee wananchi.
ü Utetezi wa haki – anashambulia mavua ya
jamii.
ü Bidii – anafanya juhudi kuoana watoto wa kike wamesoma
ü Utu – anamtembelea mangwasha ili kumjulia hali.
ü Malezi – anawalea wanawe vizuri.
ü Mapenzi – anawapa wanawe mapenzi
ya wazazi wote wawili baada ya
mkewe kufariki Uwajibikaji – anawaleta polisi kulinda mali ya wenyeji
wa
Matango
ü Siasa – angombea kiti cha kua
mtemi
c) Eleza jinsi mwandishi alivyotumia mbinu ya sadfa katika riwaya
ü Ni sadfa Mangwasha kupitia ofisini mwa mrima na kumpata Sagilu.
ü Ni sadfa kwa wanabiashara kukutana na watuwalioanzisha moto usikui sadfa Sagilu kumtembelea Mangwashawakati ambapo anhitaji kubwa la pesa kuwanunulia mawnawe sare
ü Ni sadfa Mangwasha kupata dirisha ambalo halikungwa kanisani
ü Sadfa inawakutanisha Mrima na Magwasha katika ofisi ya chifu na kuanza kuchumbiana
ü Ni sadfa kwa sukari, chumvi na mafuta kuisha pamoja mwezi unapokariba
ü Waketwa wanapiga gari la sihaba msako na kupata vijikaratasi vya kuwahamisha
ü Ni sadfa mbungulu kumtembelea rafikiye kisha anapata zilipo Red Bead Lodgings.
ü Lonare anatekwa nyara siku ambayo walinzi wanaacha kumlinda
ü Ni sadfa Lonare kupatikana siku ya kupiga kura