• Tamaa ni hali ya kutaka sana kitu, matamanio ya kitu au jambo. Tamaa kama hamu au utashi mkubwa wa kufaidi kitu huwa mbaya iwapo utafaidi mtu mmoja kutokana na ubinafsi wake au kundi la watu lenye maslahi yanayofanana.
• Ubinafsi hubainika pale mtu anapojipendelea yeye au kujifikiria yeye mwenyewe bila ya kuwajali wengine. Kuna wahusika kadha wanaoendeleza maudhui ya tamaa na ubinafsi hasa pale
Mwandishi anataja kuwa mtaa wa Majuu ulikuwa umeshiba ubinafsi na ubaguzi.
Mtemi Lesulia anajawa na tamaa ya uongozi. Yuko tayari kuwadhulumu au hata kuwaua wapinzani wake kutokana na tamaa ya uongozi wa nchi. Anamteka nyara Lonare asiweze kuwa katika kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu anapohisi kwamba huenda akamshinda na kuwa mtemi (uk.10, 51, 164-172).
Mtemi Lesulia, Sagilu na Mbwashu wanahujumu pato la nchi kutokana na tamaa ya kujilimbikizia mali.
Ubinafsi wa Mtemi Lesulia unaonekana pale anapomiliki rasilimali za serikali hasa kupitia kwa unyakuzi unaoendelezwa na mkewe Nanzia.
Nanzia anaonyesha tamaa na ubinafsi pale anapojaribu, kubinafsisha jumba la Skyline Mall ambalo ni mali ya serikali (uk. 147) na ardhi ya Matango kwa kushirikiana na mafisadi wenzake.
Sagilu anaendeleza maudhui ya tamaa na ubinafsi pale utashi wake wa pesa unampofanya kuhodhi bidhaa kama vile ngano ili kuiuza kwa bei yajuu (uk. 17). Ubinafsi wake unamfanya Sagilu kuwazuia wengine wasimpiku kibiashara. (uk. 16).
Ubinafsi pia unamfanya Sagilu kumtumia Mrima ili kujinufaisha kisiasa kutokana na tamaa ya uongozi.
Sagilu aliandamwa pia na tamaa za kimwili. Anawabadilisha wanawake hadi kuitwa dudumizi kutokana na kuvizia na kuwachukua wake wa wengine (uk. 18).
Anaendeleza maudhui ya tamaa anapomnyemelea Mangwasha tangu pale alipokuwa msichana hadi baada ya kuolewa na Mrima ili kutosheleza uchu wake.
Tamaa ya Sagilu inamfanya hata kuzaa na mke wa Mtemi Lesulia kutokana na udhaifu uliodhihiri katika ndoa yake.
Mrima anaendeleza maudhui ya tamaa na ubinafsi pale ambapo tamaa ya pesa inamtosa katika tabia potovu. Anadanganywa na Sagilu huku akipewa pesa hadi kuitelekeza jamaa yake.
Ubinafsi wa kuyajali maslahi yake pekee unamfanya kukaidi masharti ya ndoa na uwajibikaji.
Ubinafsi wa Mafamba unamfanya kuhujumu sheria za nchi kwa kuutetea ufisadi serikalini.
Ubinafsi pia unamfanya Mafamba kudanganya korti kuwa vyeti vya kumiliki ardhi vya wenyeji wa Matango vilikuwa ghushi (uk. 94), na kwamba serikali ilitaka kujenga soko katika mtaa wa Matango.
Tamaa ya pesa inamfanya Sihaba kujiingiza katika biashara ya ulanguzi wa watoto wa kike (uk. 141-144).
Usuhuba wa Sihaba na Sagilu pia unajengwa juu ya misingi ya tamaa ya pesa na ubinafsi aliokuwa nao Sihaba.