Nguu za Jadi; Maudhui ya Utamaduni

• Utamaduni ni ujumla wa maisha ya watu. Aina mbili za maudhui ya utamaduni zinajitokeza katika riwaya hii.

• Kuna utamaduni wa kiasili ambao unazingatia jadi na desturi za kiasili za jamii zinazozungumziwa, na ule unaokumbatia usasa.

 Mangwasha anapotamani kuondoa uhasama wa Wakule na Waketwa lakini kwa vile yeye ni mwanamke, hangeweza kusikilizwa.

 Jamii ya Mangwasha pia haimtarajii kuwa na ujasiri wa kwenda kuongea na wakuu wa nchi na sio tu kwa sababu ya hali yake ya kijamii lakini pia kutokana na hali ya kuwa yeye ni mwanamke (uk. 8).

 Utamaduni unamfanya mwanamke kuonekana kama chombo tu cha kuchuuzwa na mwanamume (uk.10) pale ambapo baadhi ya Waketwa waliochomewa nyumba zao wanatoa hoja kuwa kuna wale waliowauza wake zao kwa wakuu ili wapate ajira.

 Kulingana na Mangwasha wanawake walipaswa kusikiliza na kutenda bali si kusikilizwa na kutenda." (uk. 11).

 Mangwasha anatujulisha kuwa utamaduni uliomlea ulimfunza kutotumia sifa za kike kustarehesha wanaume ili kujinufaisha kimaisha.

 Kulingana na Mangwasha, utamaduni unamfunza mke kujitegemea katika maisha bali si kumtegemea mume kujikimu katika maisha yake (uk. 12).

 Mhusika Mbungulu anasema kuwa mila na tamaduni hazimruhusu mwanamke kumfuata mumeo kwenye makao ya starehe." (uk. 32).

 Kulingana na Mrima, mke hapaswi kumuuliza mumewe kule aendako au atokako. Mrima anasema,

 Mrima anasema kuwa yeye ni mwanamume na mke hangemzuia kuoa; kwamba angeweza kuoa wakati wowote na idadi yoyote ya wanawake.

 Mrima anasisitiza kuwa mila haimruhusu kutunzwa na mkewe ndio maana anachelea kurudi nyumbani kwa sababu hakuwa na kazi ya kuikimu familia.