Hii ni tabia inayodhihirisha ukosefu wa huruma. Ukatili unatokana na moyo mgumu kiasi cha kuweza kutekeleza mauaji au kuleta hasara na mateso kwa wengine.
Sagilu ambaye aliweza hata kuwaua washindani wake katika biashara (uk. 16).
Ukatili wa Sagilu unabainika pia pale anapoagiza maziwa ya watoto yenye sumu bila kujali maisha Yao.
Sagilu anapomtesa Mangwasha kimawazo huku akihatarisha ndoa yake kwa kutumia pesa kumlewesha Mrima hadi akawa mlevi na mwishowe kuachishwa kazi.
Sagilu anaendeleza maudhui ya ukatili anapompokonya mwanawe mpenzi wake na hivyo kuuvunja uchumba wao.
Kushiriki kwa Sagilu katika kupanga njama ya kuwachomea Waketwa makazi yao ili yeye na jamaa ya mtemi wafaidi kisiasa ni mwendelezo pia wa maudhui ya ukatili.
Ukatili unaendelezwa na Mtemi Lesulia pale anapowadhulumu raia wake kupitia kwa vitendo vya kikatili ili kujinufaisha kisiasa. Anampangia Lonare mauti kwa sababu za kisiasa.
Ukatili wa serikali ya Lesulia unabainika pale yeye na wenzake waliposhindwa kesi ya ardhi ya Matango, tunaona hakimu akinyang'anywa leseni ya uanasheria hata kushushwa madaraka bila kuzingatia haki na ushahidi uliowasilishwa mahakamani.
Kauli ya mtemi kwamba, "Wale panya wamesharudi katika makao Yao..." (uk. 78) inaonyesha ukatili wake kwa wenyeji wa Matango.
Maudhui ya ukatili yanaonekana wakati wa uchaguzi wa mchujo tunapomwona mtemi akiwapa vijana pesa na kuwaamuru waharibu zoezi hilo bila kujali iwapo vijana hao wangeuliwa na askari walinda usalama wala kujali rai za mwanawe Ngoswe (uk. 129- 130).
Mtemi Lesulia anaendeleza maudhui ya ukatili pale anapohusika katika kutoweka kwa Lonare siku chache kabla ya uchaguzi mkuu.
Maudhui ya ukatili yanaonekana kupitia kwa Sihaba pale anaposhirikiana na Sagilu kuwachomea Waketwa nyumba zao.
Maudhui ya ukatili yanaendelezwa na Sihaba pia pale anapowapelekea Mrima na Mangwasha zawadi ya arusi akiwa na lengo la kuwaangamiza.
Sihaba anapoanzisha makao ya Red Beads Lodgings ili kuwachuuza vigoli kwa wanaume bila kujali maisha yao ya baadaye ni mwendelezo wa maudhui ya ukatili.