1. “…anachukua vidonge vyake na kuvimeza kabla ya kuketi kwenye kochi mpya.”
(a) Weka dondoo hili katika muktadha wake. (alama 4)
Msemaji-mwandishi
Mrejelewa-Sara
Mahali- nyumbani kwa Sara
Wakati- sara ana maradhi kwa hivyo anameza vidonge
(b) Tambua aina za taswira katika dondoo hili. (alama 2)
Taswira oni- jinsi abachukua vidonge
(c) Eleza umuhimu wa mandhari ya dondoo hili. (alama 4)
Haya ni mandhari ya nyumbani kwa Sara ambayo yanadhihirisha yafuatayo:
Malezi-sara anawalea wanawe vyema
Mapenzi- sara anampenda Yona
Migogoro- kuna mtafaruku kati ya Yona na Sara.
Sifa za Yona kama mlevi, mvivu na mbabedume zinakuzwa.
Tunatanguliziwa mhusika Dina kama rafiki wa dhati wa Sara.
Utamaduni- Sara anaamini kuwa fimbo ya mzee hurithishwa mtoto wa kwanza
(d) Eleza nafasi ya mwanamke ukijikita katika utamaduni wa jamii ya “Bembea ya Maisha”. (alama 10)
Mshichana lazima aolewe. Msichana anafaa kuolewa baada ya kutimiza umri wa kubaleghe.
Msichana apewi nafasi ya kupata elimu. Kizazi cha jana hakikudhamini elimu ya mwanamke. Sara anasema elimu kwa mtoto wa kike ilikuwa bezo. Mwanamke anafaa kutii mumewe. Ni utamaduni kwa mke kutunza mumewe. Sara anapoenda mjini, Yona anakosa wa kumtunza.
Mke anafaa kuwa mvumilivu kwenye ndoa. Sara anasalia kwenye ndoa yake licha ya madhila aliyopitia.
Mwanamke anafaa kuongozwa na mume. Bunju anasema kuwa yeye ni kichwa naye Neema awe shingo.
Zamani mabinti walienda unyagoni na kufunzwa jinsi ya kutunza familiazao na waume zao. Sara alieleza haya.
Utamaduni ulikandamiza msichana. Utamaduni wa jadi haukumruhusu mtoto wa kike kwenda shule. Sara anaeleza kuwa hakupata nafasi ya kusoma.
Mwanamke anawekewa laana sisizo na misingi yeyote. Sara anaenda kulala kwa Asna licha ya chumba chake kuwa kidogo.
2. “Wakati mwingine maisha haya hukufanya kijisikia kama abiria kwenye gari liendalo kwa kasi. Unatamani dereva apunguze mwendo lakini unakumbuka kuwa safari bado ni ndefu na hutaki kufika ukiwa umechelewa. Basi unatulia japo ndani una wasiwasi, hutulii. Lakini huwezi kushuka maana safari itaganda. Kwa hivyo, unajitahidi tena, japo wakati mwingine unajikuta umetambaliwa na uchovu, shaka na tuhuma.”
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
Msemaji- Neema
Msemewa-Bunju
Mahali- sebuleni mwao
Wakati- hii ni baada ya Buju kumdokezea kuwa hawezi kumsaidia na hela za kumtibu mamake na jinsi ni laana kukaa na wakwe kwa nyumba moja.
(b) Changanua mtindo katika dondoo hili. (alama4)
Tashbihi- kijisikia kama abiria kwenye gari liendalo kwa kasi.
Jazanda/ istiara- safari bado ndefu-maisha bado ni marefu na yana mengi
Tashihisi-umetambaliwa na uchovu, shaka na tuhuma
(c) Dhihirisha umuhimu wa mzungumziwa wa maneno haya katika kuijenga tamthilia ya “Bembea ya Maisha”. (alama 6)
Huyu ni Bunju
Anaendeleza migogoro katika ndoa. Anatofautiana na mkewe kuhusiana na malezi ya mwana wao Lemi. Anasema mume hafai kutumwa na mkewe. Anadhihirisha sifa za mkewe Neema kama mkarimu kwa kuwa alitumia mshahara wake kumlipia dadake Asna karo chuoni na kuishi pamoja na Salome kwao nyumbani.
Anaendeleza ploti-kupitia mbinu rejeshi, anadokeza alivyompata Neema akiwa mahututi.
Anakuza maudhui ya elimu. Anawalipia wanawe karo. Anamlipia shemeji yake Salome karo pia.
Anawakilisha wanaume ambao ni wawajibikaji kwani anamjengea babake nyumba, kuwapa chakula, mavazi, kulipia wanawe karo na kumnunulia mkewe gari.
Ni kielelezo cha watu watamaduni kwani anadai kuwa mama mkwe hafai kulala kwake kwani ati ni laana.
Anatumiwa kuonyesha uhuru ulioko katika ndo za kisasa. Anamruhusu mkewe kutumia mshahara wake apendavyo.
Anawakilisha wanaume wababedume. Anaona yeye ni mwanaume na ndiye kichwa cha familia, anastahili heshima, hastahili kupewa majukumu na mkewe kama kumtembeza mtoto wao Lemi.
(d) Eleza namna maisha yanamfanya mzungumzaji “kujisikia kama abiria kwenye gari liendalo kwa kasi”. (alama 6)
Mamake Sara ana amaradhi ya moyo.
Hana hela za kutosha kumtibu mamake Sara, anamuomba mumewe usaidizi.
Ana kazi nyingi kule kazini-anasema kazi hizo ni kama safari ya ahera.
Anakosa muda wa kumlea mwanawe Lemi. Malezi amemuachia yaya Bela.
Anakosa muda wa kumpeleka mwanawe matembezini.
Wana mivutano katika ndoa na mumewe kuhusu malezi, mila na majukumu.
Ana wajibu wa kushughulikia wazazi wake –kuwaajiria wafanyakazi.
3. a. Changanua mtindo katika kifungu kifuatacho (alama 10)
‘‘Mwanangu usitake sana kuhoji alacho kuku. Utachafukwa roho umchukie kuku bure. Wala usitake kujua nyuki ameitengenezea nini asali. Hutaila. Maadamu yameshakuja,yapokee. Mtoto akinyea kiganja hakikatwi wala hatuulizi kwa nini. Ni maumbile. Maumbile hayo,sawa na vidole, hayafanani. Sawa na watoto wachezeao bembea, tumeicheza na tungali tunaicheza sehemu yetu kwa zamu. Haidhuru iwe ya kamba au chuma. Muhimu ni kwamba tumeshirikiana kusukumana kwenye bembea ya maisha. Upo wakati inakuwa raha tele na upo wakati inakatika na kutubwaga. Hiyo ndiyo raha hasa ya maisha. Ni sawa na chombo kinachomenyana na mawimbi katika bahari. Hutufanya kuwa macho katika safari…”
Mtindo
Usemi halisi “mwanangu….
Msemo- Kuchafukwa roho
Jazanda- kuku, nyuki, Kamba, chuma, bembea
Sentensi fupifupi-Hutaila.
Mdokezo wa methali- yameshakuja, yapokee
Taswira- mtoto akinyea kiganja.
Takriri- Maumbile, maumbile.
Usambamba- sawa na vidole hayafanani, sawa na watoto
Kinaya- raha unapobwagwa na bembea.
Tashihisi- chombo kumenyana na mawimbi.
Mdokezo- safari…
b. Fafanua namna mandhari ya dondoo hili yalivyochangia usukaji wa tamthilia. (alama 10)
kuchimuza maudhui
kuchimuza dhamira
kujenga ploti Kuchimuza wahusika.
kuchimuza sifa zao (wahusika)
kuchimuza mahali na wakati wa tukio kuchimuza njia ya kusuluhisha mgogoro ule
Tan: maelezo ya mandhari lazima yakite mizizi katika dondoo pekee wala si kitabu kizima
4. ‘‘Walishasema baada ya dhiki ni faraja, Faraja ni zao la dhiki. Leo hii kikapu cha mama kimejaa ndago.”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
Msemaji ni Dina
Alikuwa anamwambia kwa Kiwa
Walikuwa myumbani kwa Dina.
Dina anataka kumuonyesha kuwa Sara alikuwa amepitia shida nyingi.
b) Eleza vipengele viwili vya kimtindo kwenye dondoo. (alama 4)
Methali-baada ya dhiki ni faraja
Jazanda- leo kikapu cha mama kimejaa ndago
c) Eleza maudhui mawili yanayodokezwa kwenye dondoo. (alama 2)
Mabadiliko- kitambo Sara na familia yake walipitia dhiki na sasa hivi wana faraja.
Uvumilivu- Sara ni mtu ambaye alivumilia dhiki nyingi na baadaye zikampa faraja.
d) Eleza sifa za msemaji.(alama 5)
Msemaji ni Dina
Mwenye moyo wa huruma: Sara anapougua, Dina anamsaidia kazi za nyumbani na kumpa moyo kuhusu ugonjwa alionao.
Mwenye ujirani mwema: Anapoitwa na Sara amsaidie kupikia bwana yake, anafika nyumbani mwa Sara kumsaidia katika shughuli hiyo.
Mwenye roho safi: Hana kinyongo chochote kwa watoto au familia ya Sara. Anafurahia kufanikiwa kwa watoto wa Sara.
Mwenye mapenzi ya dhati: Anamsaidia rakifi yake Sara kwa dhati.
e) Kwa kutolea mifano mwafaka eleza dhiki alizopitia mama ambaye sasa kikapu chake kimejaa ndago. (alama 5
Kukosa watoto na kusemwa na wanajamii
Kukosa mtoto wa kiume na kusemwa na majirani
Mumewe (Yona) kuingilia ulevi na kumdhulumu.
Anaachiwa jukumu la malezi
Anapata maradhi ya moyo kutokana na mateso ya mumewe.
5. (a) ‘Hizo juu-chini chini-juu ndizo utamu wake. Ni kama maisha kwa jumla. Yana pandashuka ndiyo lakini pandashuka hizo ndizo hutupa kuridhika hatimaye tunapozishinda.’ Thibitisha kuwa maisha yamejaa pandashuka ukirejelea tamthilia: Bembea ya Maisha (alama 10)
Sara alikuwa buheri wa afya alipoolewa na Yona. Baadaye anapata ugonjwa wa moyo kutokana kupigwa na Yona.
Sara na Yona wanakaa muda mrefu bila mtoto. Wanasimangwa na kudharauliwa na wanajamii. Hata hivyo, wanajaliwa Neema, Asna na Salome
Yona aliyekuwa mwalimu hohari baadaye anafutwa kazi kutokana na ulevi.
Elimu ya mtoto wa kike haikuthaminiwa katika enzi za kina Sara. Sasa inathaminiwa kwa kuwa binti zake Yona wamesoma na kuhitimu
Sara anapougua na kushindwa kupika, Dina anakuja kumsaidia kupika
Wazazi wa kijijini walijilelea watoto wao na kuwaadilisha kwa mfano, Sara.Wazazi wa sasa kama Neema wanakosa muda wa kutosha na watoto wao kutokana na kazi nyingi.
Yona anatelekeza majukumu yake ya nyumbani baadaye anaepa kumsaidia mkewe katika kazi za nyumbani kama kupika.
Sara anasema kuwa barabara za mjini zilikuwa mbovu. Siku hizi zimesakafiwa na usafiri umekuwa wa haraka.
Watoto wa Dina zamani walikuwa maskini sasa wana afadhali
Sara anapougua Neema anampeleka hospitalini. Anatibiwa na mwishowe akapona.
Nduguze Neema (Salome na Asna) wanapokosa karo, Neema anawalipia hivyo kuendeleza masomo yao.
Neema anamtumia baba yake (Yona) pesa za kununua dawa. Hata hivyo, Yona anatumia pesa hizo kwenda kwa wazee wenzake ili asionekane shabiki.
Yona anapofutwa kazi watu wanawatenga na kuwaita maskini wa fedha lakini mwishowe Neema anamsaidia.
Mwanzoni Yona hakuweza kuelewa athari ya ugonjwa wa Sara lakini baadaye anaelewa na kuwa tayari kumsaidia.
Yona alikuwa wa kwanza kuingia chuoni kijijini mwao lakini anamalizia kuwa mlevi hodari jambo linalomfanya kushindwa kufanya kazi.
Asna anaona kuwa ndoa ina mitihani chungu nzima ambayo haina silabasi mahususi, hata hivyo, Sara anampa ushauri kuwa si ndoa zote zina changamoto na kumtia moyo aolewe.
Zamani Neema alikuwa anaona kuwa baba yake hakuwathamini yeye na wanuna wake lakini baadaye anagundua kuwa baba yao (Yona) anawapenda na kuwathamini.
(b) ‘Umenirudisha nyuma kweli katika siku zile za ujana wangu. Asubuhi niko skuli majira ya alfajiri…’’
(i) Eleza mbinu ya kimtindo inayojitokeza katika dondoo hili.
Mbinu rejeshi / Kisengerenyuma – umenirudisha nyuma kweli
(ii) Fafanua mifano mingine minane (8) ya matumizi ya mbinu hii katika tamthilia (alama 8)
Mifano zaidio ya mbinu rejeshi:
Dina aneleza kuhusu maisha ya awali ya familia ya Yona na Sara ambapo walipata masimango kwa kukosa mtoto.
Yona anakumbuka wakati alipokuwa mwalimu alivyokuwa akibeba vitabu vya wanafunzi kwa baiskeli ili kuvisahihisha wikendi.
Neema anakumbuka namna usafiri wa zamani ulivyokuwa mgumu kabla ya maendeleo ya teknolojia. Safari iliyochukua siku tatu sasa inachukua saa chache tu.
Bunju anasema kuwa zamani Neema alikuwa anamheshimu lakini sasa heshima hiyo imepungua.
Dina anamkumbusha Kiwa namna Yona alikuwa akimtesa na kumpiga Sara hadi anapoteza fahamu.
Bunju alimwachia Neema mshahara wake ili awasaidie wazazi wake na kumwelimisha Asna.
Kupitia kwa mbinu hii, tunapata kujua kwa Salome aliwahi kuishi na familia ya Neema na kwamba alipata ufadhili wa kwenda ng’ambo.
Asna anasema kuwa zamani watoto wa Dina walidharauliwa kwa kuwa maskini, tofauti na alivyo sasa.
Zamani Yona alipenda dini. Baadaye aliacha dini na kuwa mlevi baada ya kushinikizwa na wenzake chuoni.
Sara anakumbuka zamani akiwa angali mzima na afya yake.
Sara anamkumbusha Yona kuwa alipokuwa na afya yake walishirikiana kutafuta riziki ya kuwalea watoto wao.
Sara anakumbuka namna ambavyo Bunju aliokoa maisha ya Neema.
Neema anakumbuka namna Bunju alivyompata barabarani katika ajali mbaya.
6. “Mwenyewe ona ulivyokonda kama ng’onda!”
(i) Yaweke maneno haya katika muktadha wake.
Haya ni maneno ya Sara.
Anamwambia Asna
Walikuwa chumbani mwa Asna kule mjini
Baada ya Sara kuona jinsi ambavyo Asna alivyokuwa akikumbwa na changamoto nyingi mjini na kumtaka arudi kijijini naye Asna akakataa kwa kuwa alikuwa ameelimika na kutaka kujitegemea binafsi.
(ii) Tambua mbinu mbili za lugha katika dondoo hili. (alama 4)
Tashbihi – konda kama ng’onda!
Nidaa -Ng’onda!
(iii) Eleza umuhimu wa msemaji wa maneno haya. (alama 6)
Umuhimu wa Sara:
kielelezo cha mlezi bora- anatoa ushauri kwa watoto wake
Anaonyesha uvumilivu. Maradhi yamemfanya akonde sana lakini anavumilia
- alivumilia mateso ya mumewe Yona
-alivumilia masimango ya watu alipokuwa hana watoto na alipopata wasichana tu.
Anadumisha utamaduni wa jamii ambapo mwanamke anafaa kumtumikia mumewe Kila wakati- nafasi ya wanawake katika jamii.
Anaendeleza maudhui ya ugonjwa
Anaendeleza maudhui ya ndoa
Anaendeleza maudhui ya utiifu- alikuwa mtiifu kwa mumewe Yona
(iv) Fafanua umuhimu wa mandhari ya dondoo hili.
Kuonyesha mkengeuko- Asna amekengeuka
Kuonyesha changamoto za ndoa: - kati ya Neema na Bunju - Kati ya Sara na Yona
Kuonyesha ushauri nasaha unaotolewa na Sara kwa Asna
Nafasi ya mwanamke katika jamii – wapishi bora
Malezi- Sara alivyowalea watoto wake
Elimu na changamoto zake- Asna kutopata kazi, anaishi kwenye SQ
Kazi- Asna anafanya kazi ya vibarua
Mandhari ya mjini mabadiliko/ mkengeuko- watu wa mjini wanastahabu kukonda ili wapendeze.
7. a) Changanua mtindo katika dondoo lifuatalo. (alama 6)
(Anajisemea) “ Bunju ni mmoja wenu. Nyote ni wanangu.” Hayo ni maneno ya mama. Wakati huo sikuona. Sasa ninaona. Wanasema mwenye macho haambiwi tazama. Kweli ilioje! Japo hutokea wakati tukalalamika, ninafikiri Bunju ni zawadi nzuri kwetu. Leo tungekuwa wapi bila Bunju? Maji yangezidi unga. Hebu fikiri ! umepata ajali mbaya. Inakuacha mahututi. Anapita mtu katika gari lake. Anakufanyia mpango wa flying doctors, ndege inafika kukupeleka hospitali.
Uzungumzi nafsia ;alikuwa anajisemea
Litifati ;anarudia maneno kama yalivyonenwa na mamake ,’Bunju ni mmoja wenu.nyote wanangu’
Mbinu rejeshi; anarejelea wakati uliopita ‘wakati huo sikuona
Methali _mwenye macho haambiwi tazama
Nidaa ;kweli ilioje! Hebu fikiri
Swali balagha ;leo tungekuwa wapi bila Bunju ?
Msemo –maji yangezidi unga
Kuchanganya ndimi_flying doctors.
Utohozi ;hospitali
Taswira ;ajali mbaya inakuacha mahututi
b) Kwa kurejelea tamthilia ya Bembea ya Maisha jadili changamoto saba zinazoikumba asasi ya ndoa. (alama 14)
Kichapo –Yona anampiga mkewe Sara.
Utasa /kukosa mwana_Sara na Yona wanakosa watoto kwa muda mrefu hadi wakasengenywa
Masengenyo- walisengenywa na kuitwa tasa na wagumba
Vitisho- Yona aliwashikia mkwaju wanawe.
Magonjwa –kutokana na kichapo Sara alipata ugonjwa wa moyo
Kelele –Yona angepiga kelele kila siku
Matusi na masimango –Yona alimtusi mkewe Sara
Upweke -Sara alibaki pweke mumewe akienda ulevini, Yona alibaki peke yake Sara alipoenda mjini
Tofauti za kimtazamo –Neema na Bunju walitofautiana kuhusu ukale na usasa
Kukosa mtoto wa kike aliyedhaniwa ndiye mrithi halisi
8. “Maji yangekuwa yamewafika shingo basi wangeshindwa kuishi pamoja. Ndoa ni bembea.”
a) Fafanua muktadha wa dondoo hili.
Anayezungumza ni Sara
Anamzungumzia Asna
Nyumbani kwa Asna
Anazungumzia ndoa ya Neema, Asna anaposema hataki kuolewa kwa kuwa ndoa haina mema
b) Bainisha tamathali moja ya usemi inayojitokeza. (alama 2)
msemo –maji yangekuwa yamewafika shingoni
jazanda –ndoa ni bembea
c) Eleza sifa nne za msemaji wa maneno haya. (alama 4)
Mvumilivu –alivumilia katika ndoa licha ya vichapo na matusi.
Mwenye bidii –anafanya ukulima
Mwenye huruma –anamhurumia Yona kwa kazi zilizomlemea nyumbani. Mshauri –anamshauri Asna kuhusu ndoa na Neema kuhusu ulezi.
Mwajibikaji –kabla ya ugonjwa alikuwa akimpikia mumewe vizuri
Mdhamini ndoa –alivumilia hata baada ya kusengenywa na wanakijiji kwa kukosa watoto hapo awali.
Mlezi mwema –alitafuta riziki ya familia yake Yona alipozama ulevini
Mwenye shukrani –anamshukuru Dina kwa kumsikiliza anaposhtakiwa kwake.
Mwenye kujinaki/kugigamba/majivuno –anasema Lemi ana akili za kwao. Mtamaduni –anasema kuwa mtoto wa kiume ndiye hurithi fimbo ya mzee wala si wa kike
d) Mwandishi wa Bembea ya Maisha ameshughulikia suala la uwajibikaji kwa kina. Thibitisha. (alama 10)
Yona anafanya kazi zote ; kutoa ng’ombe zizini, kushughulikia kuku na kuandaa kiamsha kinywa.
Neema anawanunulia wazazi wake jiko la gesi.
Bunju anawajibika kama mwanamme. Anajenga nyumba na kutafutia familia yake riziki.
Madaktari wa hospitali alikolazwa Sara wamewajibika, wanadumisha usafi.
Sara na Asna wanaenda hospitalini kumuona mama yao.
Neema anawalipia ndugu zake karo.
Bela anafika kazini mapema kilasiku.
Kabla ya ugonjwa, Sara alikuwa anapika na kumkaribisha Yona ale.
Neema anakipamba chumba chao kiasi cha Bunju kusema chapendeza mno.
Bunju anafanya mpango wa Flying Doctors kumpeleka Neema hospitalini kwa ndege anapopata ajali.
Neema anapeleka mamake hospitalini kupata matibabu kisha anamrudisha nyumbani mwenyewe.
Asna anampikia mamake chakula kitamu.
9. “Mwanangu binadamu mchoyo kwa lake lakini mkarimu ajabu kwa la mwenziwe. Atakukarimu kwa la mwenziwe na atakupa nyongeza usiohitaji lakini lake atalizika katika giza la kina cha moyo wake. Ndiyo hulka yake mwana wa Adamu.”
a) Eleza muktadha wa maneno haya.
Maneno ya Dina.
Anamwambia Kiwa.
Yuko nyumbani kwa Dina.
Dina alikuwa akimwambia Kiwa kuhusu yale magumu ambayo Sara ameyapitia katika maisha
b) Jadili namna chanya msemaji na wenzake wajinsia ya kike walivyosawiri wakati ka tamthilia ya Bembea ya Maisha. (alama 6)
Mwanamke ni karimu k.m Neema anatumia mshahara wake kulipia karo Asna na Salome.
Mwanamke ni mwenye bidii k.m Salome amesoma na kuhitimu first class.
Mwanamke ni mwajibikaji k.m Neema anamwendea mamake kijijini ili kumpeleka hospitali.
Ni mwenye utu k.m Dina anaenda kumsaidia Sara kwa upishi.
Mwanamke ni mtiifu k.m Bela anaitika anapoitwa na Sara na kuagizwa kuamka mapema.
Mwanamke ni mwenye busara k.m Sara anamshauri Neema kuwa maisha ya ndoa ni bembea.
c) Fafanua umuhimu wa mazungumzo kati ya msemaji na msemewa katika tamthilia ya Bembea ya Maisha (alama 10)
Yanachimuza maudhui ya uwajibikaji k.m Kiwa amekuja kumjulia hali mamake.
Yanadhihirisha sifa za Sara k.v uvumilivu k.m anapoitwa tasa anavumilia. Yanaonyesha maudhui ya changamoto ya ndoa k.m Dina anasema Sara alikaa kwa muda kabla ya kujaliwa motto.
Yanaonyesha sifa za Neema wakati Kiwa anasema ana akili kama za simaku.
Yanachimuza maudhui ya umbea k.m wanajamii walimsema sana Sara.
Yanaendeleza ploti ya hadithi.
Yanaonyehsa Yona kama mwenye msimamo dhabiti.
Yanaonyehsa maudhui ya nafasi ya mwanamke. Ni mnyonge.
Yanaonyesha sifa za Dina kama mdadisi k.m anamuuliza mwanawe kwa nini amekonda.
Yanakuza maudhui ya mila na utamaduni k.m jamii inashinikiza Sara apate mtoto wa kiume wa kumrithi.
Yanachimuza falsafa ya mwandishi ya kupinga tamaduni zinazothamini mtoto wa kiume na kumdunisha wa kike.
Yanaonyesha mgogoro kati ya Yona na jamii huku ikimtaka azae mtoto wa kiume na kumrithi.
10. Jadili maudhui yafuatayo kwa kutolea mifano maridhawa kama yanavyoshughulikiwa katika tamthilia ya Bembea ya Maisha.
a) Mabadiliko
Ni hali ya kutoka katika hali moja hadi nyingine.
Yona alikuwa akiwanyoosha viboko wanafunzi lakini sheria ikabadilika kwamba siku huwezi kumnyoosha mtoto kwa kiboko.
Tofauti na hapo awali Yona ataka kuzitumia siku zake za uzee kumshughulikia mkewe.
Yona alikuwa mzuri lakini akageuka na kuwa mlevi.
Mtazamo kuhusu mtoto wa kike kutazamwa kama asiye na haki ya kurithi unabadilishwa na kizazi cha leo.
Zamani wasichana wakiozwa punde wanapobuleghe lakini ziku hizi wanaolewa wakitaka.
Zamani Yona hangepika lakini tunamwona akiandalia familia yake kiamsha kinywa – utamaduni kubadilika.
Uk. 72 Neema anabadilisha mtazamo wake kuhusu babake.
Bunju anabadilisha mtazamo wake wa kutomsaidia Neema katika matibabu ya Sara – sasa anasema atampiga Jeki. Afya nzuri ya Sara kubadilika na kuwa duni.
Jamii inabadilika na kuiheshimu familia ya Yona – ambayo ilikuwa ikidharauliwa hapo mbeleni. Alama 10
b) Migogoro
Kati ya kizazi cha jana na kizazi cha leo k.m katika ndoa.
Migogoro ya kitamaduni kati ya Asna na mamake – kuhusu babake kuchota maji kisimani.
Kitamaduni kati ya Asna na Sara. Sara anaamini kuwa msichana aolewe tu anapobaleghe.
Tamaduni- Bunju dhidi ya Neema, Asna na Bela. Bunju haamini wazazi kulala nyumbani kwa mkwe.
Migogoro kati ya Sara na Yona ambapo Yona anampiga Sara kwa kukosa mtoto wa kiume.
Kati ya Neema na Bunju kuhusu majukumu ya kifamilia-matibabu ya Sara.
Neema na Bunju wanavutana nani ampeleke Lemi Ziara.
Bunju anasema Neema anapenda kukana na kubishana, jambo ambalo litamfanya kuonekana mbwa kasoro.
Mgogoro kati ya jamii ya Yona na ile ya Sara baada ya Sara kutojaliwa na mtoto.
Mgogoro wa familia ya Yona na Sara unakuzwa na kuwa wa kijamii-inayomlaumu Yona kwa kukosa mtoto wa kiume.
11. ``Walishasema, baada ya dhiki ni faraja, Faraja ni zao la dhiki. Leo hii kikapu cha mama kimejaa ndgo.”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
Msemaji ni Dina
Msemewa ni Kiwa mwanawe Dina
Pahali ni nyumbani kwa Dina
Tukio ni kuwa Dina anamjuza Kiwa kuwa Sara alikuwa amepitia shida nyingi
b) Tambua vipengele vya kimtindo katika dondoo hili. (alama 2)
Methali - baada ya dhiki ni faraja.
Jazanda - leo kikapu cha mama kimejaa ndago(kumaanisha kuna mabadiliko). (2x1=2)
c) Bainisha maudhui mawili yanayodokezwa katika dondoo hili. (alama 4)
Mabadiliko - kitambo Sara na familia yake walipitia dhiki lakini sasa wana faraja.
Uvumilivu - Sara ni mtu aliyevumilia dhiki nyingi na baadaye akapata faraja.
d) Eleza sifa za msemaji. (alama 5)
Msemaji ni Dina.
Mwenye moyo wa huruma - anamsaidia Sara na kazi za nyumbani na kumpa moyo kuhusu ugonjwa alionao.
Mwenye ujirani mwema - anaitikia wito wa Sara na kumsaidia shughuli za nyumbani.
iii) Mwenye roho safi - hana kinyongo chochote kwa watoto/familia ya Sara. Anafurahia kufanikiwa kwa watoto wa Sara.
Mwenye mapenzi ya dhati - anampenda mwanawe Kiwa; pia anamsaidia rafiki yake Sara kwa dhati.
Mcha Mungu - kauli zake nyingi zinarejelea Mungu kwa mambo mengi.
Ni mfariji - anamfariji Sara. Anamwambia kuwa atapona.
Mwenye utani - anamtania Sara kuwa labda anapanga kusafiri kwa ndege maana hajamtuma kukata tiketi.
e) Fafanua dhiki alizopitia mama ambaye kikapu chake kimejaa ndago. (alama 5)
Kukosa/kuchelewa kupata watoto na kusemwa/kusengenywa na wanajamii.
Kukosa mtoto wa kiume vilevile akasemwa na majirani kuwa hawana mrithi.
Mumewe anaingilia ulevi na kumdhulumu/kumpiga.
Anachiwa jukumumzigo wa kulea watoto na kuikimu familia kwa jumla.
Anapata maradhi ya moyo kutokana na mateso ya mumewe Yona.
12. Ukilazwa tayari unakuwa umeonja seli. Hata wahudumu wenyewe hawana mlahakamwema. Amri na vitisho kama askari. Unashindwa kama uuguze moyo ama ugonjwa. Katika wodi hewa iliyojaa harufu ya dawa imezagaa, vitanda vimesalimu amri mpaka shiti zikagura. Yaani hali nzima haikupi matumaini ya kutoka ukiwa bora. Matumaini yanadidimia. Tumaini lako unaliweka sala.
a) Fafanua muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
Msemaji ni Asna
Wasemewa ni Sara na Neema
Pahali ni hospitalini mjini..
Mazungumzo ni kuhusu hali duni za hospitali za vijijini
b) Tambua toni mbili katika kifungu hiki. (alama 2)
Toni ya kutamauka - hali nzima hospitalini haikupi matumaini ya kutoka ukiwa bora.
Toni ya huzuni - matumaini yanadidimia. Tumaiani lako unaliweka katika sala
c) Chambua mbinu za kimtindo katika kifungu hiki. (alama 5)
Taswira mnuso - hewa iliyojaa harufu ya dawa imezagaa.
ii) Utohozi - seli, shiti wodi.
Tashbihi - amri na vitisho kama askari.
Nahau/msemo - vitanda vimesalimu amri.
Tashihisi - vitanda vimesalimu amri; shiti zikagura.
d) Eleza namna mandhari ya dondoo hili yalivyochangia kujenga hadithi Bembea Ya Maisha. (Alama 9)
Yanalinganisha huduma duni za afya kijijini na huduma bora za afya mjini.
Yanatusaidia kuelewa maudhui ya uwajibikaji kupitia kwa wahudumu wa hospitalini za mjini.
Yanachimuza pia maudhui ya uongozi mbaya hospitalini kijijini.
Yanachangia katika kuonyesha sifa za wahudumu wa hospitalini mjini ni wenye bidii na watiifu.
Yanasaidia kuonyesha sifa za wahudumu wa hospitalini kijijini kama wezembe na dhalimu.
Yanachimuza matatizo yanayokumba hospitali za mashambani kama vile uchafu, uhaba wa vitanda vizuri, shiti n.k.
Yanachangia mtiririko wa vitusi, vile Sara anapofika hospitalini kupata matibabu.
Yanakuza sifa za Asna kama mdaku.
Yanajenga sifa za Neema na kumsawiri kama mtu mwadilifu.
Yanachimuza mbinu za kimtindo kama vile utohozi,tashbihi, taswira n.k.
13. "... wakati mwingine mwindaji huwa mwindwa. Hata kijijini wanaishi watu . Watu hao hawakumbwi na dhiki kiasi hiki. Ya nini kung'ang'ana kuyatafuta maisha kama kwamba hayapiti? Maisha ni mshumaa uso mkesha! Ukijiachia sana peupe hata upepo unaweza kuuzima kabla ya kulika hadi nchani.” a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
Msemaji ni Sara
Msemewa ni Asna
Walikuwa nyumbani kwa Asna/servant’s quarter.
Sara ana maoni kuwa Asna angehamia kijijini kumsaidia.
b) Bainisha toni katika kauli hili
Toni ya kushauri- Maisha ni mshumaa uso mkesha
c) Eleza vipengele vinne vya kimtindo alivyotumia msemaji kufanikisha uwasilishaji wa ujumbe.
Methali-mwindaji huwa mwindwa
Swali ya balagha- ya nini kung’ang’ana kuyatafuta maisha kama kwamba hayapiti?
Nidaa- Maisha ni mshumaa uso mkesha!
Jazanda/ sitiari- Maisha ni mshumaa uso mkesha( maisha ni mafupi na hayapo daima)
Mdokezo - …wakati mwingine
Tashihisi / uhuishi - upepo unaweza kuuzima kabla kulika hadi nchani.
kweli kinzani – mwindaji – mwindwa
msemo/nahau - Maisha ni mshumaa uso mkesha!
d) Eleza umuhimu wa msemaji katika kuendeleza ploti ya tamthilia hii.
Sara ametumiwa kuonyesha athari ya migogoro katika ndoa. Maradhi ya moyo anayogangua ni tokeo la mzozano baina yake na mumewe Yona.
Kupitia kwake tunaona alivumilia ndoa yake na kufanya juu chini ili wanawe wapate elimu ili kuboresha mustakabali wao.
Aidha, anahakikisha kuwa binti zake Neema na Asna wanapata elimu.
Ni mfano wa wanawake wenye bidii. Hata akiwa hospitalini, akili yake inafikiria mazao yake aliyoyaacha shambani.
Kupitia mazungumzo baina yake na Asna, yanamsawiri Asna kama kijana aliyekengeuka kiasi cha kutotaka kuingia katika ndoa.
Kupitia kwake tunaelezwa kuhusu usuli wa kutopika. Sara anaeleza kuwa kwa sababu ya ugonjwa wake hangeweza kupika.
Sara alisemwa na kutukanwa na wanajamii kwa sababu ya kuwapata watoto wa kike pekee. Hii ilipelekea Yona kuingilia ulevi.
Baadhi ya matukio katika maisha ya wahusika fulani yanaangaziwa katika nyumba yake. k.m Dina anaangaziwa kama mwenye utu kwani anaenda kumpikia kwa kuwa alikuwa mgonjwa.
Kupitia mazungumzo baina yake na Yona, tunapata kujua kuwa Neema ndiye aliyewasomesha wanuna wake hadi chuo kikuu.
Pia, Sara anatujuza kuwa Neema ndiye aliyewaajiri wafanyakazi nyumbani kwake.
Ametumiwa kuonyesha uwajibikaji wa Neema. Neema anagharamia matibabu ya Sara na pia anampa babake/Yona pesa za kwenda kwa wazee wenzake.
Kupitia kwake tunafahamu kuwa Bunju ndiye aliyemsaidia Neema baada ya kupata ajali na kulipia gharama za hospitali ilhali Bunju hakuwa amemjua Neema.
Kupitia mazungumzo baina yake na Neema na Asna tunapata kujua kuhusu tofauti baina ya hospitali za mjini na kijijini. Huduma za hospitali mjini ni mzuri lakini za kijijini zinalinganishwa na seli na wahudumu hawana mlahaka mwema.
Hatima ya mgogoro baina ya Sara na Yona. Yona anaachana na mila na tamaduni za kutopika kwa Mwanaume.
Anaonyesha jinsi utamaduni ulivyowakandamiza wasichana –Sara anamwambia Asna kuwa siku zao elimu ya wasichana ilifanyiwa bezo na kuwa Sara aliachia darasa la saba.
Kuonyesha mustakabali wa Sara wa kumsamehe,Yona-Yona anamwomba Sara msamaha kwa kuwa hakujua upeo wa ugonjwa wa moyo.
14. (a) Fafanua umuhimu wa mazungumzo kati ya Luka, Beni na Yona katika kujenga tamthilia ya “Bembea ya Maisha”
Yanaonyesha sifa ya Luka kuwa ni mkarimu -anawakaribisha wenzake kwake nyumbani kwa chakula cha mchana na kinywaji.
Kuonyesha mila na utamaduni - Luka anadokeza kuwa kitendo cha kula pamoja kwa wazee kilikuwa kinafanywa na wazee wao kwani mavuno ya kwanza huonjwa na wazee na kutoa baraka. (uk. 58)
Yanachimuza ukengeushi - Beni anasema kuwa tatizo la watu siku hizi ni kuzitupa mila zao kabisa. (uk.58) Wajukuu wa Yona hawafahamu lugha yao ya asili. (uk-59)
Yanadhihirisha mchango wa dini - Yona anaeleza dini,imechangia watu kuona mila kuwa chafu. (uk.58)
Yanaonyesha mabadiliko katika malezi - Yona anaambia wazee wenzake kwa malezi kule mjini yameachiwa kina yaya. (uk.59)
Yanaonyesha jinsi mila na tamaduni zilikuwa kandamizi kwani hazikuruhusu mtoto wa kike kuenda shule au kuridhi kitu – kulingana na Luka.(u.k 60)
Yanadhihirisha jinsi hao kina Luka walivyomshinikiza Yona kuoa mke mwingine apate mtoto wa kiume.(u.k 60)
\ Yonadhihirisha sifa za Beni jinsi ana wivu kwa watoto wa Yona kwani hataki Luka awataje katika mazungumzo yake.
Yanachimuza ufanisi wa watoto wa Yona – Luka anasema walikuwa nyota ya jaha. Neema anarudi kijijini akiwa na gari.
Yonaonyesha thamani ya mtoto wa kike ilivyopanda na nafasi yake kupanuka kwani zamani walikuwa wakiwategemea waume zao laikini sasa hali ni tofauti(u.k.60)
Yonaonyesha maudhui ya uhafidhina – Luka anamuona Neema kama si wao tena baada ya kuolewa.
Yanachimuza hekima ya Luka – Luka anamuuliza Beni kuwa lipi muhimu kati ya tiba au mtu kuja kumpikia mwenzake? (uk.61)
Yanaonyesha sifa za Yona hapo awali kuwa alikuwa mualimu mwenye bidii - Yona anasema angefika kazini majira ya alfajiri, kiboko mkononi, siku nzima kazi tu, aliweza kufunga vitabu kwenye baskeli kwenda kuvisahihisha wikendi. (uk. 62)
Yanadhihirisha mabadiliko katika nyanja ya elimu - Yona anasema siku hizi huwezi tena kumnyoosha mtoto kwa kiboko. (uk.62)
Yanachimuza athari za pombe - jinsi pombe ilivyomfanyaYona kuwa mtumwa akashindwa kuishi bila kulewa (uk62)
Yanaonyesha uvumilivu au stahamala za Sara wakati Yona alipokuwa mlevi. Yona anasema Sara alimsaidia kulea na kusomesha watoto na kwamba bila yeye chombo kingezama. (uk-62)
Yanaonyesha jinsi Yona alivyoanza kutumia tembo alipokuwa chuoni. Wenzake walimpa mvinyo kumrai kuonja. (uk. 62)
Yanadhihirisha uongo wa Beni- kuwa mtoto wake ni fundi wa mitambo na wala si injinia. (uk. 63)
Yanaendeleza ploti- tunatambulishwa kuwa Luka,Beni na Yona ni marafiki na walishiriki vileo pamoja.
(b) "Bembea inapolika na kukatika haiwi mwisho wa michezo.Huungwa na mchezo kuanza tena." Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa kutolea mifano mwafaka tamthiliani.
Neema nusura apoteze uhai wake katika ajali Lakini Bunju akamnusuru kwa kumpeleka hospitalini.
Neema na Bunju baada ya kugombana kuhusu mchango wake Bunju katika matibabu ya Sara, Neema anaamua kumuelewa Bunju hivyo ndoa yao kuendelea vyema.
Baada ya changamoto ya kutopata watoto iliyoyumbisha ndoa baina ya Sara na Yona, hatimaye walijaliwa watoto watatu.
Maradhi ya moyo yalipomlemea Sara kiasi cha kukata tamaa na maisha, Neema anajitolea kuhakikisha mamaye amepata matibabu murua hivyo kumrejeshea matumaini.
Japo Yona na Sara walikosa mwana wa kiume na kusimangwa na wanajamii, mabinti zao wanakuwa wembe masomoni hivyo kuwapa furaha katika ndoa yao.
Neema alipoonekana kukata tamaa kutokana na kile alichokiona kuwa ni ubahili wa Bunju, Sara alimpa wasia uliompa nguvu zaidi katika ndoa yake. Yona baada ya kugundua kuwa ulevi wake unaangamiza familia yake, anaapa kutolewa tena na kumhudumia mkewe Sara.
Yona na Beni walipotofautiana kuhusu watoto wao,Luka anafaulu kutuliza hali na wazee hawa kuendelea na sherehe zao.
Baada ya kumsababishia mkewe maradhi ya moyo,Yona anamwomba Sara msamaha kwa kuwa hakujua upeo wa ugonjwa wa moyo.
Mgogoro baina ya Sara na Neema kuhusu Yona unaisha Neema anapogundua upendo wa Yona Kwao anapoacha utamaduni wa kutopika chakula.
Mgogoro baina ya Sara na Yona unaisha. Yona anapoachana na mila na tamaduni za kutopika kwa mwanaume.
Tatizo la Sara la kushindwa kumpikia mkewe linasuluhishwa na jiraniye Dina anapokuja kumsaidia.
15. Asubuhi niko skuli majira ya alfajiri, kiboko mkononi. Anayekuja baada yangu hata kama hajachelewa ana lake.
a) Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4)
Haya ni maneno ya Yona
Akimjibu Beni
Wamo kwa Luka nyumbani
Beni alikuwa amemkubusha zama zile akiwa mwalimu alikuwa na nguvu za kujipikia
b) Tambua mbinu mbili za mtindo katika dondoo hili (alama 4)
Kisengere nyuma-anaeleza alivyokuwa akifika asubuhi na mapema na kuwaadhibu walio chelewa alipokuwa mwalimu
Utohozi- skuli
Taswira- kiboko mkononi
Kinaya-kuadhibu mtoto ambaye hajachelewa
c) Bainisha toni inayojitokeza katika dondoo hili (alama 2)
Toni ya majigambo/kiburi/majivuno/majitapo
d) Fafanua sifa mbili za msemaji kutoka kwenye dondoo (alama 2)
Mwenye bidii- anarauka asubuhi na mapema kwenda kazini
Katili- aliwaadhibu hata wasiochelewa waliofika baada yake kufika.
Mwenye majitapo/kiburi- 2x1=2
e) Onyesha jinsi elimu ilivyosawiriwa katika Tamthilia Bembea ya Maisha (alama 8)
Elimu ina gharama; Sara anaambia Yona kulipia elimu ya Chuo kikuu si lelemama. Jambo hili limewashinda hata wanaume wenye mishahara minono serikalini (uk. 1), Shule ya bweni anakosomeaMina inagharimu pesa nyingi(uk.27).
Elimu inamsaidia mwanamke kuolewa; Yona anamwambia Sara kwamba Neema hangepata ndoa ikiwa hangejinyima mengi ili kumwelimisha(uk.2). Elimu hupalilia vipawa; Bela anaambia Dina kuwa Lemi huimba na kucheza shuleni;Lemi amwonyesha Bela minenguo na miondoko waliyoifanya shuleni (uk.22).
Wazazi huthamini alama na nambari wanayoshikilia watoto katika mitihani; Neema anaona ni heri Lemi ameongeza alama ilhali Bunju anasema afadhali angepunguza alama lakini apande nafasi darasani (uk.26).
Shule huwa na wanafunzi wa viwango tofauti kimasomo; Neema alikuwa mwerevu darasani nao watoto wa Dina wakawa hawaitikiwi na elimu japo walijawa hekima na nidhamu.
Elimu hufinyanga maadili;Lemi huendesha mambo yake kwa udhu na adabu. Hutuzwa mara nyingi kwa kuwa kubeli(uk.26).
Vijana wameelimika lakini hawana ajira; Asna hana kazi licha ya kuwa na shahada.
Bidii ya Salome masomoni inamsaidia kupata ufadhili wa kuendeleza masomo ng’ambo(uk.28).
Elimu inawakengeusha vijana; Asna anahiari kuishi mjini bila kazi kuliko kurudi kijijini;anaona akirudi kijijini watu watamshangaa(uk.31).
Elimu ya wasichana ilipuuzwa zamani, ilidharauliwa; Sara aliachia masomo darasa la saba akaolewa
Ni wajibu wa wazazi kusaidia wanao kusoma; Neema anamsaidia Lemi kusoma(uk.47), Bunju humsaidia Lemi kufanya homework (uk 49).
Elimu humsaidia binadamu kuishi na kutatua matatizo yake; Sara anamwambia Asna kutumia elimu waliyompa kutegua mitego ya ndoa na kuendesha maisha yake(uk.53).
Ulevi huathiri utendakazi wa walimu;Yona anakosa kuwajibika hadi anafutwa kazi (uk. 56).
Elimu ni chombo cha maendeleo na ufanisi; Neema anarudi kijijini akiendesha gari safi (uk.61).
Walimu walitumia kiboko kurekebisha wanafunzi wakati Yona alipokuwa mwalimu. Leo sivyo.
Vijana hushinikizwa na marika kuingilia ulevi;Yona alishinikizwa na vijana wenzake chuoni kuingilia ulevi. Watoto wanafaa kupelekwa shule bora(boarding) inayotia matumaini zozote 8x1=8
16. Kumbuka mrina haogopi nyuki. {kimya} Marehemu mama yangu alizoea kutuambia kuwa nguvu hazimwishi mwanadamu wala hazipotei bure; humalizwa tu na mabuu. Mwanangu, usifanye hofu. Nikujuavyo mimi, hukuingia katika bahari si yako. Wala hakuna refu lisilokuwa na ncha. Yote yana mwisho eti! Ipo siku yote yatapita. {kimya} Mkulima hodari libasi yake huwa imechakaa na kuchoka lakini moyoni anabaki safi kama theluji kwa kutosheka na tija ya sulubu zake. Huwezi kumlinganisha na mkulima wa nguo safi zilizopigwa pasi zikanyooka.
a) Changanua mtindo katika kifungu hiki (alama 6)
Methali-mrina haogopi nyuki,/ hakuna refu lisilokuwa na ncha.
Kisengere nyuma- marehemu mamangu alizoe kutuambia…
Jazanda- bahari
Tashhisi- libasi yake huwa imechoka na kuchakaa
Tashbihi- safi kama theluji
Kinaya- mkulima wa nguo safi
Taswira- nguo kuchakaa/ nguo safi
Nidaa- yote yana kikomo eti! Zozote6x1
b) “Mila na desturi zetu zimewajenga hivyo walivyo na sisi hivi tulivyo”. Imani na itikadi huthaminiwa sana na jamii zetu. Jadili ukweli wa kauli hii kwa kurejelea tamthilia ya bembea ya Maisha (alama 10)
Yona anaambia Sara kuwa fimbo ya mzee(majukumu) hurithi mtoto wa kwanza(uk, 2).
Dina anaambia Kiwa watu waliuliza na wanauliza nani atarithi ardhi ya Yona
Yona anataka kujua sababu ya Sara kutomwandalia chochote(uk. 13)' Sara anaambia Dina mila imewafanya wanaume kuwaachia wanawake kazi zote za nyumbani.
Sara anaambia Dina watu wakijua mume anamsaidia mke jikoni watasema hadhi yake imeshushwa, kwa mizani ya jamii mwanamke atakuwa amejivua nguo (uk. 14).
Neema anamwambia Bela kuwa wazee wake hawawezi kulala kwa mkwe wao (uk. 24).
Wazazi waBunju walipokuwahaihawakuwahi kuja kuishi kwake(uk.29).
Bunju anaambia Neema kuwa hawezi akakaa na wazazi wa Neema kwake, ni laana.
Sara anaambia Asna kuwa ikiwa Yona ataonekana akiteka maji kisimani kijiji kitasema kwamba amewasomesha watoto ambao wamemweka Sara jijini ili Yona ataabike; watamdharau(uk 45).
Luka anaambia Yona na Beni kuwa zamani ilikuwa ni desturi mavuno ya kwanza kuonjwa na wazee ili kutoa baraka(uk.58).
Sara anaambia Neema binti za mama anayemzuia mumewe kufanya atakayo (anayemtilia mguu wa kausha) hawaolewi, huzeekea nyumbani (uk. 66).
Sara anamwambia Neema utamaduni haumruhusu mwanamke kushindana na mwanamume
Kulingana na Sara, hekima si hekima itokapo kwa mwanamke(uk. 68).
Wanawake ni wategemezi kwa waume zao.
c) Onyesha jinsi msemewa hakuingia katika bahari si yake (alama 4)
Msemewa- Neema: (mwanafunzi aangazie mafanikio ya Neema)
Licha ya kuwa msichana anafaulu kuchukua fimbo ya Yona kwa kuwasaidia yeye na mamake Sara.
Anaweza kusoma na hata kuwashinda wanaume.
Anafanikiwa kupata kazi na kutomtegemea mumewe kwa kila jambo.
IV. Alifaulu kuendesha gari mjini jambo lililowashinda wanaume.
Anafaulu kumsomesha Asna hadi chuo kikuu jambo lililowashinda wenye mishahara minono.
Anafaulu kugeuza fikra za mumewe za kutosaidia wakwe zake
Anafulu kujengea wazazi nyumba